Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Morogoro, Kuhani Zangina S Zangina, kipindi cha Uandikishaji Wananchi katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura 2025 alitembelea maeneo mbalimbali ya Manispaa akianzia Ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini na kufika kwenye Kata.
Mwenezi Zangina alipita kwenye Vituo vya Uandikishaji, Nyumba za ibada na Vijiwe vya madereva bodaboda ili kuangalia mwitikio wa Wananchi na kujaribu kuzibaini changamoto zilizopo katika zoezi la Uandikishaji
Maeneo aliyopita Mwenezi CCM Mkoa wa Morogoro ni pamoja na vituo mbalimbali ndani ya Kata ya Chamwino (Mtaa wa Visegese, Mtaa wa Mwembeni, Mtaa wa Mwande, Mtaa wa Napome, Mtaa wa Mgulasi, Mtaa wa Mahita, Mtaa wa Msufini, Mtaa wa Tupendane, Mtaa wa Malipula); Na, Kata ya Kihonda Maghorofani ikiwemo (Mtaa wa Kitata, Mtaa wa Kitata, Mtaa wa Ngerengere, Mtaa wa Maghorofani B, Mtaa wa Maghorofani A, Mtaa wa Bima, Mtaa wa Airport,)
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika maeneo mbalimbali aliyopita Mwenezi Zangina aliwaomba viongozi wa makundi na taasisi husika wawasihi watu wao na Waumini wao wajiandikishe kwenye Daftari la Mpiga Kura ambao nao pia walionekana kulipokea kwa furaha.