Mwenge wa uhuru utafutiwe nishati mbadala ya kuuwezesha kuwaka badala ya kutumia mafuta ya taa na utambi unaotoa moshi

Mwenge wa uhuru utafutiwe nishati mbadala ya kuuwezesha kuwaka badala ya kutumia mafuta ya taa na utambi unaotoa moshi

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Bila shaka kichwa cha habari kinajieleza vizuri sana.

Binafsi sina tatizo na falsafa ya uanzishwaji wa mbio za mwenge wa uhuru. Tatizo langu kubwa ni namna wanavyoweza kuathiri afya za wanaoukimbiza.

Nishati inayotumika sio rafiki kwa afya za wanaoukimbiza na hata walio karibu nao mahali unapowasili.

Kama tunavyofanya jitihada za kuzuia matumizi ya kuni na mkaa kwa kupikia, vivyo hivyo tujitahidi kubuni njia mbadala ya kuufanya mwenge wa uhuru uweze kutoa mwanga. Vijana wanateseka sana na moshi.

Naomba kuwasilisha.
 
hahahaha ukitumia nishati mbadala unakua umekiuka masharti ya mganga..... hilo pembe la ng'ombe lazima lipite kila kijiji lisambaze tb nanukimwi muendelee kufa kama panya
 
Nadhani hata baba wa taifa angekuwepo,angeshauri tuendane na mabadiliko ya sayansi na teknoljia kwa kubuni nishati mbadala
 
Bila shaka kichwa cha habari kinajieleza vizuri sana.

Binafsi sina tatizo na falsafa ya uanzishwaji wa mbio za mwenge wa uhuru. Tatizo langu kubwa ni namna wanavyoweza kuathiri afya za wanaoukimbiza.

Nishati inayotumika sio rafiki kwa afya za wanaoukimbiza na hata walio karibu nao mahali unapowasili.

Kama tunavyofanya jitihada za kuzuia matumizi ya kuni na mkaa kwa kupikia, vivyo hivyo tujitahidi kubuni njia mbadala ya kuufanya mwenge wa uhuru uweze kutoa mwanga. Vijana wanateseka sana na moshi.

Naomba kuwasilisha.
View attachment 3058976
Naunga mkono hoja, nami niliwahi kuzungumza hiki kitu, Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?. humo nilishauri tufanye research ya wakimbiza mwenge wote, walikufa na umri gani na walikufa kwa maginjwa gani?, mtashangaa!. Wakati mbio za mwenge zinabuniwa hatukuwa na nishati safi, lakini sasa tuna methene, haina moshi, tuna propane haina moshi, tuna gesi ile ya kupikia, tuna gesi asili, tena unaweza kukuta kununua vimitungi vidogo vya LNG kuwashia mwenge ni cheaper kuliko sumu ya butane tunaowavutisha vijana wetu mwisho tunakuja kuwaua kwa slow death, by the time wanakufa ni many years after no one remembers walikuwa wakimbiza mwenge!.

Niliwahi kumshauri yule Blaza wangu Ingekuwa ni Amri Yake, Magufuli Angefutilia Mbali Mbio za Mwenge!, Jee Ni Amri ya Nani?!.

Basi tuu,
Enzi za ujana maji ya moto, nilishiriki sana mikesha ya mwenge na yatokanayo
P
 
Mimi naungana mkono na wale wazalendo wengine wanaoshauri huo mwenge kuwekwa kwenye jumba la makumbusho. Maana sioni kama una tija yoyote kwenye dunia yetu hii ya leo.

Kiufupi umepitwa na wakati.
 
Mwenge una faida gani?
Faida za mwenge zipo japo ni chache kulinganisha na hasara.

Mojawapo ya faida ni kutoa fursa kwa wajasiamali kuuza bidhaa zao mahali mwenge utakapokeshea.

Pia unasaidia kutoa ajira kwa vijana wanaoukimbiza.

Falsafa ya mwenge imebeba maudhui mapana kwa taifa. Yaani tunapozungumzia matumaini, upendo na heshima!

Ingawaje, kwa sasa maeneo mengi mwenge umebaki kuwa wa viongozi wa maeneo husika. Hasa mahali ambapo utapita kuzindua miradi.

Labda tupendekeze njia gani itumike kukagua na kuzindua miradi mbalimbali badala ya kusubiri mwenge.
 
hahahaha ukitumia nishati mbadala unakua umekiuka masharti ya mganga..... hilo pembe la ng'ombe lazima lipite kila kijiji lisambaze tb nanukimwi muendelee kufa kama panya
Hivi panya huwa wanakufa kwa ukimwi pia?
 
Faida za mwenge zipo japo ni chache kulinganisha na hasara.

Mojawapo ya faida ni kutoa fursa kwa wajasiamali kuuza bidhaa zao mahali mwenge utakapokeshea.

Pia unasaidia kutoa ajira kwa vijana wanaoukimbiza.

Falsafa ya mwenge imebeba maudhui mapana kwa taifa. Yaani tunapozungumzia matumaini, upendo na heshima!

Ingawaje, kwa sasa maeneo mengi mwenge umebaki kuwa wa viongozi wa maeneo husika. Hasa mahali ambapo utapita kuzindua miradi.

Labda tupendekeze njia gani itumike kukagua na kuzindua miradi mbalimbali badala ya kusubiri mwenge.
Lakini pia suala la kamati za wilaya kupanga aina za miradi itakayokaguliwa na kuzinduliwa na mbio za mwenge; linasababisha kuficha miradi yenye ubadhilifu. Wanakwepa tuhuma za ufisadi na rushwa.
 
Kwanini unasema hivyo?
Inasemekana kuwa walioasisi Mwenge ni Wachawi sita nguli ili kuwapumbaza Watanganyika.

Walipata agizo hilo toka kwa Shetani siku waliyomzindika Nyerere na taifa huko Bagamoyo, Mwaka 1961.
Wachawi hao waliongozwa na Jichawi Nguli,
👉Mzee Forojo Ganze, Master, aliyeenda kuonana na kuongea na Lucifer ana kwa ana, kwa kutumia lugha mbali mbali za kijini.

Baada ya kufikisha huo ujumbe kwa Nyerere, Master Ganze alikata roho.
{Walienda na Nyerere, walivyo maliza kumzindika alirudi akawaacha huko Bwagamoyo.
Na Kuna siku aliongea kuwa walimwambia aruke shimo walilochimba huku likiwaka moto kwa chini}

Zindiko hilo lilishilikisha wachawi Nguli wengine Watano.
2. Primius Mubanga Julius
3. Shaibu Kalole Mtiga
4. Mfaume Golo Tumbo
5. Muhammedi Abubakar Musindamba.
6. Shehe Yahaya Hussein

Hicho kikosi ni kizito haswa, kikitaka kumwita Shetani Lusifer ili kuongea naye anakuja fasta huku akitetemeka kwa woga.
 
Back
Top Bottom