Mwengine tena ajiua Mbeya, kuna shida gani kwa vijana wa Mbeya ?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
933
Reaction score
3,051
Ughonile watu wa Mbeya, nipo Njombe (zamani ikiwa shemu ya Iringa) nimekuwa nikistuka kwa visa vya mara kwa mara kwa vijana wa Mbeya kujiua. Kunakoelea sio, ni muda wa kujadili shida ilipo ipate suluhisho.

Mwezi uliopita dereva bajaji mkazi wa kata ya Iganzo, Jijini Mbeya alijinyonga majira ya saa 1 jioni kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni ugumu wa maisha, Marehemu aliacha mke na mtoto mmoja wa miezi mitano.

machi 4 mwezi huu kijana mwengine alijinyonga chumbani kwake majira ya saa sita mchana wakati mkewe akifua nguo nje ya nyumba waliyopanga, Marehemu aliacha mke na watoto watatu.

March 7 kijana mwingine kutoka Josephat jijini Mbeya amejiua kwa kunywa sumu ya kukausha magugu shambani na kabla ya kufanya tukio ulimtumia ujumbe baba yake akimueleza kuna jambo litatokea

 
Amejinyonga au amenyongwa?

Matukio hayo yanaweza kuwa ni targeted crime, huwezi kujua undani wake bila ya kufanya kwanza uchunguzi wa kina kabisa ulio huru.

Katika dunia ya leo hii kuna Mambo mengi Sana yapo yanaemdelea nyuma ya pazia.

Kumbuka: Kuna aina Kuu Mbili za Vita, Conventional War and Unconventional War!
 
wamejinyonga, sababu zikiwa changamoto za maisha
 
Hawa watu na ndugu zao wa Iringa na Njombe wana matatizo ya kiakili, we umeona wapi mtu anashikwa na nyege usiku yuko peke yake chumbani anajiua kisa haelewi kwanini yuko singo?
 
Hawa watu na ndugu zao wa Iringa na Njombe wana matatizo ya kiakili, we umeona wapi mtu anashikwa na nyege usiku yuko peke yake chumbani anajiua kisa haelewi kwanini yuko singo?
Iringa / Njombe ni story iliyopata umaarufu ya Mkwawa ila haya mambo nadra sana, mikoa ya kaskazini kama Geita kumepashika moto
 
Iringa / Njombe ni story iliyopata umaarufu ya Mkwawa ila haya mambo nadra sana, mikoa ya kaskazini kama Geita kumepashika moto
Whaat, kule nako mtu akishikwa na nyege anajiua kama jamaa wa Iringa, Njombe, Mbeya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…