sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,001
Nisiku nyingine tena,
Kuna walioamka na hasira huku wengine wakiamka na furaha. Ndio, nazungumzia watu waliokuwa kwenye foleni za usaili wa ajira za muda katika zoezi la sensa.
Binafsi nilishiriki usaili huo Kama msailiwa niliyeomba moja Kati yanafasi zilizotangazwa.
Wakati unasubiriwa muda wa usaili ufike,watu walijijusanya kwa vikundi huku wakiongea stori mbalimbali walizoona zitawasogezea muda wa kusubiri.
Makundi mawili ya wasailiwa; kundi lakwanza ni wenye ajira serikalini ama binafsi na kundi lingine wasio na ajira popote.Kila mmoja anaitaka kazi!
Malalamiko yachinichini yalitawala maongezi kwenye makundi haya.Wenye ajira wanadai hawa wasio na ajira wamekuja kuziba riziki zao kwan kwa maelezo yao wanaamini kazi Kama hizi nizao tangu zamani.
Wasio na ajira walikuwa wanalalamika kwamba watu wenye ajira ni wa binafsi,walafi,wenye tamaa na wasio nahuruma.Walitoa hoja zao ambazo kimsingi Mimi nilizielewa.
Moja Kati ya hoja zao nikwamba hii ajira ni yamuda tu hivyo wenye ajira wangewaachia wasio na ajira ili walau nao wagange njaa.
Kisanga kikazuka baada ya fununu kupatikan kwamba kipaombele Nikwa wasio na ajira.
Waombaji wenye ajira zao walikunja sura kwa kiwango kikubwa.Wanataka wao ndo wapewe kipaombele.
Kwa kutumia haki kila aliyeomba nakuitwa Kwenye usaili lazima ashindanishwe na uamuzi utolewe sawa bila kujalisha muombaji ana kazi gan nyingine.Kwa kutumia busara huenda wasio na ajira ndo walitakiwa wapewe kipaombele zaidi iwapo watakidhi vigezo.
Swali langu;Itumike haki au busara?
Wasalaam!