Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?

Mkuu, kwanza nikuulize kama ulielewa vipi kauli ya Hayati Mwalimu Nyerere kwa marehemu jaji Mark Bomani alipopeleka jina lake kwenye mchujo katika mchakato uchaguzi wa 1995 kwamba " tangu lini Jaji akawa raisi" na jaji Mark Bomani akakatwa?

Pili, kuhusu hili la DP world kwa kawaida uchumba ukiishaidhinishwa na maandalizi kuanza pamoja na hiyo mahari, ndoa inokusudiwa huwa yatangazwa hadi katika vyombo vya habari na makanisani na kwingine. Hivyo public huulizwa kuwa "Ikiwa kuna mtu yoyote kwenye zuio la haki watu hawa wasiungane katika ndoa ni lazima ajitokeze"

Sasa, weye wadhani ni kwanini hatua hii yarukwa hatua 400 na wengine kukamatwa kisha kutungiwa mashtaka?
 
Unaonaje ukanyamaza kulinda heshima yako Kwa sababu kazi za binge ni 3
Yaan kutunga Sheria, kuisimamamia serikali na kuwawakilisha wananchi.

Hakuna kitu makubaliano
 
Na Bunge walikaa kujadili makubaliano?
Bunge letu kupitisha makubaliano ni issues, limefanya uhuni tuu, na tumelizungumza hapa Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? na hapa Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
Spika alisema ni mkataba au ni vitu viwili tofauti. Hii barua yako ya uchumba na ndoa iliyojadiliwa bungeni. Mayala wakati wewe unahangaika kupigia debe hii barua amini kuna watu weshapokea na mahari kabisa. Na bibi harusi keshakabidhiwa kwa mmewe
Nilisema kila kitu hapa Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
P
 
Niliwahi kusoma sehemu, kuwa, kuna, watu wanaitwa SPIN Doctors! Hawa kazi Yao, ni, kuipotosha, story, au, kuleta, sintofahamu kwenye story, kutia chumvi na propaganda, mpaka maana ya, story inabadirika, kwa, heshima, niliyonayo kwako mkuu, naomba, usije na wewe ukswa spin doctor wa ccm!
 
Mkataba huu wa Kimangungo unasema ( Ibara 4 (2) Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari, inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini ndio basi.Hapa tayari ni dharau, yaani nchi huru ikaombe ridhaa Dubai, Tena kwa Mali zake? Kero nyingine ya mkataba huu wa Kimangungo ni kugawa bandari za Tanganyika tu na kuacha za Zanzibar, Kwani wao hawataki kunufaika? Ni kichefuchefu Hadi hasira inapanda.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
IGA sio mkataba ni makubaliano tuu ya maandalizi ya HGA. HGA ndio mkataba, hivyo kukitokea mgogoro kwenye HGA ndio utapelekwa ICSID kuamuliwa!. Uelewa ni tatizo kubwa kwa wengi wetu.
P
Kwa nini kuwe mgogoro in the first place wakati ni makubaliano tu ambayo sio enforceable by law? Mgogoro utokee wapi ikiwa kila mojawapo anaweza ku walk away kutoka kwenye haya "makubaliano" bila ya ķuwa na consequences zozote?

Usianze kutumia lugha za kudhalilisha eti uelewa ndio tatizo kubwa kwa wengi wetu ili kusudi tuogope kukupinga. Labda wewe uelewa ndio tatizo au ukada wa CCM ndio tatizo.
 
Mkuu Juan, mimi ni realist, ma realist ni wachache, kazi ya ma realist ni kuueleza ukweli halisi ulivyo hata ukiwa mchungu vipi!.
P
 
Mkuu Bwirree, hili tatizo la uelewa finyu ni kubwa kuliko, kwa post yako hii, unaonyesha wewe huijui IGA ni nini na ni ya nini, hii IGA sio mkataba, ni makubaliano tuu ya kuomba ridhaa kuingia mkataba ambao ni HGA!, IGA sio enforceable bali HGA. Hivyo mpaka hapa tulipo tukiamua to walk away, there is no consequences zozote.
P
 
Kwanza hukujibu swali nililokuuuliza.

Pili, ukisoma Part II, Article 2, Sect 1, ya IGA, inasema kwamba "the objective of this agreement is to set a legally binding framework..... " Naomba ufafanue hapa kama IGA sio enforceable by law.
 


Tatizo la mleta posa anakuwa keshalala na Dada yenu, na Dada yenu kushakula vyake, huoni kuna sababu ya kujadili maana ni mwanzo wa gundu kwa familia?
 
Nimeona TPA wamepewa cheti cha utendaji bora,kama tumeita aendeshe bandari (ZETU) huo utendaji bora ilipatikana wapi?
 
Mayala juhudi zote hizi hata U- DC umegoma kabisa !
 
Paskali, bàrua ya uchumba ina masharti yenye maswali mengi sana bila majibu.
Rejea ufafanuzi na uchambuzi wa TLS kuhusu IGA;
rejea ushauri na uchambuzi wa Prof Shivji kuhusu IGA,
Rejea uchambuzi na ushauri wa Dr. Nshala kuhusu IGA,
Rejea ushauri na uchambuzi wa TEC kuhusu IGA.
The list goes on.
Kwa msingi huu, Watanzania wengi wako tayari binti bandari "kuolewa" na DPW.
Swali, ndoa hii ni ya miaka mingapi?
Kuna vifungu vyaonesha, posa sio tu utamhusu binti bandari Dar es Salama; ni kama vile masharti ya posa yanajumuisha muoaji kuwa na exclusive rights za "kuwatokea" warembo wengine kama Tanga, Mtwara, Lindi, Tanganyika, Ng'wanza, Nyasa.
Kama mtia saini angekuwa mahsusi kwa binti mmoja tu ambae ni bandari Salama; huenda pressure ingekuwa chini.
Pale inavyoonekana binti wooote kuolewa na dume moja ambalo limekuwa na migogoro na warembo wa Djbout, Pakistan, Chile na kwingineko;.

Ndipo akili wa wenye binti wanajumbuka maneno ya Boy, "akili za kuambiwa, changanya na zako".

Ndoa hii inatukumbusha Network Group Solutions na wanaaongaza nchini;
Rite na magari Moshi;
Mikataba ya madini na mrahaba wa 3%
The list goes on.

Leo ni jumatatu; bado wakristo wengi wanatafakari bàrua kwenye mimbari jana.

Amani iwe juu ya Watanzania. Hoja zuchambuliwe na kujibiwa kwa hoja pasi kuchanganya misingi ya Imani zilizoletwa na wakoloni na wale wakipkuwepo kabla ya wakoloni (toka Ulaya) na wale waliokuwapo kabla ya ukoloni.
 
Ukiacha kutetea DP world tutakuunga mkono
Mkuu JakiDubai, kuna watu wanaandika jf ili waungwe mkono?, utaniunga mkono ili iweje?.
Anyway karibu, hili ni moja ya mabandiko yangu kuunga mkono IGA ya DPW na Bandari zetu, angalia tuu tarehe ya bandiko hili ili ulinganishe na wengine, na ikitokea una uwezo wa kusoma contents, soma contents uone jinsi ninavyoisupport DPW na Bandari zetu!.

Karibu

P
 
Kwa mfano wako huu wa binti ndo umeharibu kabisaaa! Hii kweli familia ya Mazuzu. Kwamba kuanzia binti mkubwa atakapoolewa ukitaka kuozesha binti mwingine mpaka umshirikishe mume wa binti yako mkubwa. Asiporidhia anabaki kudanga nyumbani?(4:2).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…