Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?

Kwa mfano wako huu wa binti ndo umeharibu kabisaaa! Hii kweli familia ya Mazuzu. Kwamba kuanzia binti mkubwa atakapoolewa ukitaka kuozesha binti mwingine mpaka umshirikishe mume wa binti yako mkubwa. Asiporidhia anabaki kudanga nyumbani?(4:2).
Yes Mume wa binti mkubwa yaani mkweo, kwao wana ndoa za mitala na hakuna mwiko kuoa dada na mdogo mtu!, Yakobo au Yakub aliwaoa mabinti wawili wa mjomba wake Labani, madada hao wawili ni Leah na Raheli.

Hivyo mtu aliyeoa binti yako, anakushauri kama una binti mwingine yeyote wa kuolewa, na mimi nitaarifiwe nikipendezewa pia nitume posa!.

Hivyo mahari ya binti Bandari Dar yakilamilika na binti kuolewa na kijana shababi la Kiarabu, Mwarabu wa Dubai, DPW, ikitokea tunataka kumuoza binti Bandari Tanga, Binti Bandari Mtwara, Binti Bandari Bagamoyo, Binti Bandari Mbambabay, Mwanza, Bukoba Musoma etc, tumjulishe tuu shababi DPW akipendezewa tumpe!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…