Mwenye dawa ya Kuondoa ' nuksi ' tafadhali amsaidie nayo Kocha Felix Minziro

Mwenye dawa ya Kuondoa ' nuksi ' tafadhali amsaidie nayo Kocha Felix Minziro

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Haiwezekani kila akipandisha tu Timu Ligi Kuu basi anafukuzwa.

Kaipandisha Singida United mwaka jana tena kwa taabu sana baadae wakamfukuza hakukata tamaa akajiunga na Timu nyingine na mwaka huu tena ' Mtani ' wangu huyu wa Kihaya Kocha mzoefu na Mchezaji wa zamani wa Yanga SC na Timu ya Taifa Fred Felix Minziro Kataraiya Majeshi ametoka kuipandisha Ligi Kuu kwa taabu kweli kweli Timu ya Manispaa ya Kinondoni ( KCMC ) na hatimaye leo ' ametemwa ' na sasa hajui nini cha kufanya.

Je kama ni ' nuksi ' hii aliyonayo Kocha Minziro itakuwa inaitwaje? Na je hakuna Mtu yoyote ambaye anajua Dawa nzuri ya kuondoa hii ' nuksi ' inayomuandama kila mwaka Kocha Minziro?

Nawasilisha.
 
Kama ni muislamu asali sana na aombe dua sana...hope mambo yake yatakwenda sawia.

Kuna Muislamu kabisa anayeitwa Fred Felix? Hivi hizo Bange / Bangi ambazo huwa mnazitumia kwa Kuvuta mna uhakika zinakuwaga sahihi / bora kwa matumizi ya Binadamu?
 
aje majimaji atupandishie timu yetu maana ndio analiweza. ligi daraja la kwanza imejaa mipango mingi nje ya uwanja so kibongo bongo kupandisha timu ubora wa kocha ni 35% hizi 65% ni uchawi, rushwa, fitina na marefa.
 
Sijajua mikataba yake anayosaini na timu husika imekaaje,
Sijui pia leseni yake ya ukocha ni ya daraja gani,
Malengo yake ya ukocha ni kufundisha timu za Tanzania tu au hata nje?

Makocha wetu wengi hapa nchini wanachangamoto kubwa ktk kufikia malengo yao kwa sababu:-

1.Elimu ya soka na utawala bado ni shida.

2.Leseni zao za ukocha ni madaraja ya chini & wengine wana za kuunga unga.

3.Hawataki kwenda shule/vyuo vyenye hadhi kubwa ya soka Africa, Ulaya n.k. Madaraja ya leseni ya "A" CAF, "A" au "B" Ulaya. Hata FIFA au timu za nje au ndani ya Africa zitakukimbilia kukupa mchongo maana taaluma yako ni kubwa.

4.Mikataba, Unakuwa kocha club fulani kwa muda gani, Faida ni zipi, Hasara je, Wakivunja mkataba nje ya makubaliano kinapofuata ni kipi?
Wananilipaje?, wakikataa niwashtaki wapi?
Ni mahakama za kawaida au za soka?
CAS ni nini?
Naanzia wapi kabla ya CAF & FIFA?
BMT ni nini na inahusikaje ktk hili?
Naje TFF?
Nao wakikataa niende wapi?
Wakala au mwanasheria wanahusika vipi, umuhimu wao ni upi?
 
HuyoHMrundi wa Mbao mbona hakuna la maana alilofanya MbaoM
 
Nadhani bado hajajua kazi yake ni ipi....Me nadhani kazi yake nikuzipandisha timu ligi kuu..ajitahidi akishazipandisha asepe bila kufurushwa
 
Sijajua mikataba yake anayosaini na timu husika imekaaje,
Sijui pia leseni yake ya ukocha ni ya daraja gani,
Malengo yake ya ukocha ni kufundisha timu za Tanzania tu au hata nje?

Makocha wetu wengi hapa nchini wanachangamoto kubwa ktk kufikia malengo yao kwa sababu:-

1.Elimu ya soka na utawala bado ni shida.

2.Leseni zao za ukocha ni madaraja ya chini & wengine wana za kuunga unga.

3.Hawataki kwenda shule/vyuo vyenye hadhi kubwa ya soka Africa, Ulaya n.k. Madaraja ya leseni ya "A" CAF, "A" au "B" Ulaya. Hata FIFA au timu za nje au ndani ya Africa zitakukimbilia kukupa mchongo maana taaluma yako ni kubwa.

4.Mikataba, Unakuwa kocha club fulani kwa muda gani, Faida ni zipi, Hasara je, Wakivunja mkataba nje ya makubaliano kinapofuata ni kipi?
Wananilipaje?, wakikataa niwashtaki wapi?
Ni mahakama za kawaida au za soka?
CAS ni nini?
Naanzia wapi kabla ya CAF & FIFA?
BMT ni nini na inahusikaje ktk hili?
Naje TFF?
Nao wakikataa niende wapi?
Wakala au mwanasheria wanahusika vipi, umuhimu wao ni upi?
Elimu ,elimu ,elimu...anajivunia kukaa benchi km kocha,ukiuliza atakujibu mpira Hobie yangu
 
Back
Top Bottom