Kuna mtu hapa anachanganya..anadai amewahi kuwa na Suzuki Escudo Vitara..haya magari mawili tofauti.Makes za Suzuki ni kama zifuatavyo:Escudo,Vitara,Swift,Grand Vitara,Samurai,Esteem,Verona,Reno,Xl7,Equator,Forenza,X-90,Aerio,Kizashi,Side kick,S-X4,.
Hivyo kama unataka Suzuki ni vyema ukanunua kati ya Escudo,Vitara,na Swift.haya ni magari Magumu sana .kwanza bei yake ni ndogo,vifaa vyake ni cheap na available na consuption ya mafuta ni ndogo pia kulingana na Matumizi yako.
Zamani watanzania wengi walipenda sana Suzuki Samurai ambazo halmashauri nyingi zilikuwa zinanunua pia..sababu ni hizo nilizotaja...na nyingi ni 4Wheel drive kulingana na pendekezo lako lakini.
Unaonunua gari lililotumika hakikisha vitu kadhaa mfano kwa nini muuzaji analiuza...lipo katika hali gani na je linaendana na bajeti yako?Vinginevyo usinunue gari ambalo limekuwa kero kwa mwenzio alafu akufanye wewe ndo ununue kero zake na hasara kibao.
Wengine wanapiga gari rangi au unakuta body ni Suzuki ila engine siyo Suzuki.
Ila sijaandika haya kukatisha biashara za watu ila hapa tunasaidiana mawazo.Kama unataka maelezo zaidi na unataka gari zuri .tafadhali niandikie kwa email yangu ntakusaidia kabisa na mimi ni Wakala wa Beforward.jp used cars na mimi naagiza gari ambalo utalipenda.email yangu ni;Clavingod@gmail.com.Karibu.