Mwenye Historia ya Umishenari Songea

Sema...
Tatizo la vitabu hivyo ni kuwa havina ukweli katika historia ya Tanganyika.
Waandishi wanaandika kwa kuchagua wanachokitaka si ukweli wa historia.
Swali rahisi kabisa Mzee ni imani hiyo (imani yako) iliwafikiaje hao wangoni/ wamanda huko Songea miaka hiyo?
 
Mzee hao unaowaita waislamu kupigana na hao unaowaita wakristo wa kijerumani waliupataje huo uslamu wao?
Loft...
Kwa nini unasema mimi nimewaita Waislam?
Kwani wao wenyewe wakijiitaje?
 
Swali rahisi kabisa Mzee ni imani hiyo (imani yako) iliwafikiaje hao wangoni/ wamanda huko Songea miaka hiyo?
Loftins,
Kwani Father Johannes wa Peramiho aliyewabatiza Wangoni waliohukumiwa kunyongwa na Wajerumani alifikaje Peramiho?
 
Loftins,
Kwani Father Johannes wa Peramiho aliyewabatiza Wangoni waliohukumiwa kunyongwa na Wajerumani alifikaje Peramiho?
Ina maana njia hiyohiyo iliyotumiwa na wajerumani ndio hiyohiyo iliyotumiwa hapo awali na waarabu?

Waliua na kusilimisha watu kutoka kwenye uasili wao?
 
Loft...
Kwa nini unasema mimi nimewaita Waislam?
Kwani wao wenyewe wakijiitaje?
Wangoni ni watu wenye asili ya Afrika ya kusini tunajua hii historia, na afrika ya kusini toka enzi haijawahi kuwa na population ya hata theluthi ya hiyo imani yako.

Yani kwa kifupi mzee ambacho huwa unatusimulia kuhusu uchache wa wafuasi wa hiyo dini yako England na kwingineko miaka hiyo ndio kiko S.A hadi leo hii.

Hii inaleta ukakasi sana kujua waliupataje huo uislamu wao hao wamanda/wangoni maana Songea si pwani au walifata watumwa waarabu? 🙄 maana ndio shuhuli zao hadi leo hii wale
 
Loftins,
Ushapata kusoma Across Atlantic Slave Trade?
 
Loftins,
Ushapata kusoma Across Atlantic Slave Trade?
Naaam nimepata kuisoma hii unaiamini kuwa haijachakachuliwa ila maoni ya Semahengere uliyakataa kuwa yamechakachuliwa?

😝😝
Kuna wenzako huwa wanaipinga Biblia na tukiwauliza maswali lukuki huitumia hiyohiyo kujibu hoja zetu
 
Naaam nimepata kuisoma hii unaiamini kuwa haijachakachuliwa ila maoni ya Semahengere uliyakataa kuwa yamechakachuliwa?

😝😝
Kuna wenzako huwa wanaipinga Biblia na tukiwauliza maswali lukuki huitumia hiyohiyo kujibu hoja zetu
Loftins,
Huwezi kuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwa kazi yoyote ya mikono ya binadamu kuwa imekamilika haina makosa.

Ila tofauti baina yetu hapa ni kuwa mimi nimewazidi kwa kuwa nimetafiti masuala haya na nina papers na vitabu kadhaa nilivyoandika na kuchapwa.

Kwa ajili hii basi ukinitaka rejea ya kile nilichoandika nitakupa.
 
sina nia ya kuponda lakini kusema vita ya maji maji ilikuwa ya kidini hapo inafikirisha sana, hakika huyu mtu aliyeiandika hakufanya tafiti ya kutosha.
 
sina nia ya kuponda lakini kusema vita ya maji maji ilikuwa ya kidini hapo inafikirisha sana, hakika huyu mtu aliyeiandika hakufanya tafiti ya kutosha.
Just...
Nimefanya utafiti wa kutosha na nakuwekea kipande usome nimekitoa katika kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924- 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press, London 1998.

Kipande hicho hapo chini ni kutoka tafasiri ya Kiswahili:

''Ukristo ulipingwa na Waislam tokea mwanzo.

Katika kila pambano la silaha dhidi ya ukoloni, Waislam walichukua nafasi hiyo kuwashambulia wamishionari na taasisi zao.

Waislam waliwaona wamishionari na wakoloni kama washirika wakishirikiana kupiga vita Uislam na kwa hiyo wote ni maadui.

Ukakamavu wa Uislam dhidi ya ukoloni na Ukristo una historia ndefu.

Kanisa likawa kama kibaraka likijikurubisha na kujinasibisha na ukoloni hata kuwa upande wakoloni dhidi ya majeshi ya wazalendo.

Kuelewa hali ya Uislam wakati ule, unahitaji kusoma barua iliyoandikwa na Nduna Abdulrauf Songea Mbano wakati alipokuwa akikusanya nguvu za raia wake dhidi ya majeshi ya Wajerumani na huku akijaribu kupata ushirika wa machifu wengine katika sehemu za kusini ya Tanganyika na ng'ambo ya Mto Ruvuma, Msumbiji. Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:

''Sultan Songea bin Ruuf anasema:

Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga.
Asalaam Aleikum,

Ninakuletea barua kupitia Kazembe.

Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.
Tupo katika kupigananao hapa.

Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.

Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.

Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.

Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.
Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.

Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita.

Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.

Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,

Sultan Songea bin Ruuf.''


Abdulrauf Songea Mbano
 
Kwa hiyo yule kinjekitIlie ngwale ni wa kutungwa kwenye historia mpya ya CCM...
 
Sema...
Tatizo la vitabu hivyo ni kuwa havina ukweli katika historia ya Tanganyika.
Waandishi wanaandika kwa kuchagua wanachokitaka si ukweli wa historia.
kweli kabisa...kama vita ya majimaji iko highly distorted as if walipigana wangoni tu, ilhali vita hiyo ilitapakaa karibia mikoa yote ya sasa (lidi, mtwara, mbeya,iringa,njombe rukwa na ruvuma yenyewe) lakini inavyoelezewa ni kama ilipiganwa songea tu
 
Kwenye swala la historia kila mtu anamtazamo wake kwa sababu kila kitu kipo kichwani kumbukumbu zenye ushahidi wa kweli ni chache akija mkristo ataweka yake na akija muislamu kadharika ataweka yake
 
Kwenye swala la historia kila mtu anamtazamo wake kwa sababu kila kitu kipo kichwani kumbukumbu zenye ushahidi wa kweli ni chache akija mkristo ataweka yake na akija muislamu kadharika ataweka yake
Alex,
''Kadhalika,'' si ''kadharika.''
Katika historia ya TANU kama kungekuwako na kitu miaka mingi kingeshawekwa hapa.

Mimi nimeandika historia ya wazee wangu vipi waliasisi African Association 1929 kisha Al Jamiatul Islamiyya 1933 na mwisho kuunda TANU 1954.

Historia hii ikafutwa.
Mwaka wa 1998 nikachapa kitabu hicho hapo chini kueleza historia ya jamii niliyotaka mimi.

Hakuna historia nyingine ya TANU zaidi ya hii.
Hata historai ya Mwalimu Nyerere haiwezi kushindanishwa na hii niliyoandika.

Soma kitabu cha Mwalimu kilichoandika na Prof. Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Ng'waza Kamatha tafuta ndani yake historia ya African Association na TANU.

African Association mwaka wa 1929 Nyerere ana umri wa miaka saba wala Abdul Sykes miaka mitano lakini baba yake ni mmoja wa waasisi wa African Association.

Njoo katika kuasisi TANU 1954.

Kadi No. ! Julius Nyerere na kadi hiyo kaiandika Ally Sykes (na kadi kachapa yeye Printpak kwe fedha zake), kadi No. 2 Ally Sykes na kadi No. 3 Abdul Sykes.

Historia ya TANU si ya ati ''kila mtu ana mtazamo wake,'' wala si jambo la mtazamo ni historia ambayo ina watu waliokuwapo katika nyakati hizo na wakafanya mambo kwa ushahidi.

Mchango wa Waislam ni mkubwa sana katika siasa za ukombozi wa Tanganyika kuanzia Maji Maji na ushahidi upo.

Wala huna haja ya wewe kujihisi unyonge kwa ajili ya hili.

Safari ya Nyerere UNO 1955 sherehe ya kumuaga imefanyika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika jengo la Waislam.

Huu ndiyo ukweli wa historia.
Mkutano wa Kura Tatu umefanyika Parish Hall, Tabora ukumbi wa Kanisa Katoliki.

Huu ndiyo ukweli wa historia.

 
Hivi hao Muslim's mashujaa wa vita vya majimaji walizaliwa waisilamu au walisimishwa na wakoloni wa kiarabu...
Remmy...
Ushauri wangu kwako ni kuwa jifunze historia ya ukoloni kwanza ndiyo utakuwa katika nafasi nzuri ya kujadili.
 
Mkuu umeanza kunitoa tongotongo
 
Hivi hao Muslim's mashujaa wa vita vya majimaji walizaliwa waisilamu au walisimishwa na wakoloni wa kiarabu...
Hawezi kujibu hili swali abadani.
Muislamu mweusi huwa anamuona na kumuabudu muarabu kama Mungu (mtakatifu).

Ukitaka kuyaamini haya zungumza lolote baya la kikoloni la muarabu uone kama kuna muislamu atakuwa upande wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…