Mwenye Kamusi ya Kisukuma au Kinyamwezi

Mwenye Kamusi ya Kisukuma au Kinyamwezi

Mwenye Kamusi Ya Lugha Ya Kisukuma Or Kinyamwezi Anitumie Yenye Kufundisha Lugha Vzri Na Maana Yake Wabheja
Mimi ninazo kamusi tatu za Kisukuma Kiingereza lakini nijuavyo huwezi kutumia kamusi kujifunzia lugha. Kamusi dhima yake kuu ni kukutajirisha tu upande wa msamiati (maneno) lakini sidhani kama kuna kamusi inayoweza kukuelezea muundo wa lugha kuanzia Fonolojia, Mofolojia, Sintaksia na vipengele vingine japo inaweza kuwa na vidokezo pale mwanzoni kwenye utangulizi.

Tafuta sarufi ya Kisukuma ndiyo itakusaidia japo kidogo tu. Na nijuavyo mimi hakuna kitabu cha Sarufi ya Kisukuma cha kueleweka.

Waafrika tuko wazembe kujishughulisha na lugha zetu na sasa tumezidharau nyingi zinakufa. Sana sana ukibahatisha sarufi ni ile iliyoandikwa na wamishenari walipokuja kueneza Ukristu katika miaka ya 30 - 50 huko.
 
Back
Top Bottom