Kiongozi nami niongozee Japokuwa kidogo.
Ukiwa msimbazi pale pembeni ya kituo cha polisi (tandamti st.),
nyoosha moja kwa moja na tandamti kama unaelekea sokoni mpaka ukutane na nyamwezi st. (Tandamti na nyamwezi).
Ukishavuka tu mtaa wa nyamwezi (hutoona barabara kubwa ya mtaa maana hapo ndio kuna shimo la soko la kariakoo, utaona tu uchochoro wa kwanza kulia kwako, ukienda mbele kidogo kuna uchochoro mwingine) upande wako wa kulia nadhani jengo la kwanza au la pili angalia kuna kama ngazi zinashuka chini, huko kuna mafundi wanashona sana vijora Kwa oda. Unaweza kuchukua notes kidogo kwao.
Lakini kuwa makini nao pia, huwa wanapiga pia, unaweza ukamuuliza jora moja linatoa vijora vingapi akakutajia idadi pungufu.
Ukiweza kukusanya taarifa za kutosha utafanikiwa Inshaa Allaah. Upande wa vitambaa huo huo mtaa wa tandamti yapo maduka, lakini pia kuna maduka mengi ya vitambaa mtaa wa Likoma na maeneo jirani.