Mwenye kujua Historia ya chuo cha Mlimani(UDSM)?

Mwenye kujua Historia ya chuo cha Mlimani(UDSM)?

Wana JF nani ana hii Historia ya kuanza hiki cha ya Mlimani (UDSM)

Sent using Jamii Forums mobile app
KILIANZIA PALE JENGO LA USHIRIKA LUMUMBA KARIBU MNAZI MMOJA GARDEN.

UKITOKA KARIAKOO KWENDA CLOCK TOWER.

NYERERE ALIONA UMUHIMU WA KUWA NA CHUO KIKUU HASA TATIZ LA WANASHERIA HIVYO AKAAMUA KUIFANYA LAW IWE FACULTY KITIVO CHA KWANZA.

THEN KIKAHAMIA MLIMANI. KWA KUANZIA.
 
Historia ya chuo Kikuu cha Dar es Salaama inaanza na Dar-es-Salaam University College iliyoanzishwa siku ya Jumatano tarehe 25 Oktoba mwaka 1961, ikiwa ni miezi mitatu kabla ya uhuru. Wazo la kuanzisha chuo hiki lilikuwa ni la Nyerere aliyekuwa akijiandaa kuongoza serikali ya Tanganyika baada ya uhuru huku akiona wazi kuwa kulikuwa na upungufu mkubwa sana wa wasomi wenye uwezo wa kuongonza ngazi mbalimbali za serikali. Hivyo akaanzisha chuo hiki chini ya udhamini kitengo cha External Programs cha Chuo Kikuu cha London (University of London) kufundisha sheria kwa kufuata mtaala wa Chuo Kikuu cha London, taaluma ambayo ilihitajika sana katika uendeshaji wa serikali wakati huo baada ya uhuru. Chuo hiki kilianza na wanafunzi 13 katika katika jumba ambalo baadaye lilijengwa kuwa ghorofa la Mnazi Mmoja pale mtaa wa Lumumba. Chini ya udhamini wa University of London, wahitumu wa chuo hicho walikuwa wakitunikiwa digrii za sheria za University of London, yaani LLB(London). Viongozi wa kwanza wa chuo walikuwa ni raia wa Australia A.B Weston ambaye ndiye aliyekuwa Dean wa kwanza akisiadiwa na afisa utawala mwingereza Mr Snaith. Wahadhiri wa kwanza walikuwa ni waingereza watatu: William Twinning, Patrick Mc Auslan na Sol Piccioto, mwamerika mweusi mmoja Mr Pink na mkanada mmoja Cranford Platt. Nadhani wahitimu wa kwanza chini ya Dar es Salaam University College ni pamoja na ama Mark Bomani aliyekuwa mwanasheria mkuu wa kwanza mzalendo au Justice Augustine Saidi aliyekuwa Jaji Mkuu wa kwanza mzalendo, au Julie Manning aliyewahi kuwa waziri wa sheria; sina uhakika sawasawa.

Baada ya nchi zote za Afrika ya mashariki kuwa huru, Nyerere alishauri kuwa colleges za Dar-es- Salaam, Makerere na Nairobi ambazo zote zilikuwa affiliate colleges of University of London ziungane na kuwa chuo kikuu cha afrika ya Mashariki (University of East Africa). Ni kweli wazo hilo lilikubalika na mwaka 1963, ikaundwa University of East Africa ikiwa na Colleges hizo tatu; Makerere University College ikitoa elimu ya tiba na Elimu (Medicine and Education), Nairobi University College ikitoa zaid elimu ya Uhandisi (Engineering) na Dar es Salaama University College ikitoa zaidi elimu ya sheria (Law). Nyerere akawa ndiye mkuu (Chancellor) wa kwanza na wa pekee wa chuo hicho cha East Africa, kwani baada ya yake kilivunjwa. Ndiyo maana wanasheria wengi mashuhuri wa kwanza Afrika mashariki, kwa mfano Francis K. Butagira wa Uganda, walisoma Dar es Salaam; madaktari wengi mahiri, kwa mfano Professor Makene, walisoma Makerere; na wahandisi wengi nguli mfano Professor Mshana walisoma Nairobi.

Mwaka huo wa 1963, Serikali ilihamiisha kampasi ya Dar es Salaam University College kutoka Lumumba kwenda Ubungo eneo linalojulikana leo kama Mlimani. Wakati huo eneo hilo lilikuwa limejitenga sana na sehemu nyingine ya mji, na kuwa na mazingira mazuri ya kusoma bila bugudha. Inaaminika kuwa eneo hilo lilitolewa zawadi kwa Nyerere na mzee mmoja aliyekuwa akilimiliki wakati huo, sina uhakika na stori hiyo. Kwa hiyo kuanzia wakati huo majengo mapya cha Chuo yalianza kujengwa; kuna majengo kama Nkurumah Hall yalijengwa kwa msaada wa serikali ya Ujerumani Magharibi (wakati huo) na majengo kama Hall Two na Hall Five yalijengwa kwa msaada kutoka Israeli, yalijengwa na kampuni iliyojenga Kilimanjaro Hotel (Kempinski leo), ndiyo maana yana muonekano wa kufanana structurally.

Baada ya uhuru, nchi hizi za Afrika ya Mashariki zilijisogeza pamoja kwa kipindi kifupi tu na baadaye zikaanza kutofautiana kidogo kidogo. Kwa mfano mwaka 1966, zilivunja bodi ya sarafu ya Afrika mashariki na kila nchi ikaanzisha benki kuu yake na kutoa sarafu zake. Ni vivyo hivyo kulianza kuwepo kwa figsu kwa Nyerere kuwa anatunuku digrii za Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki kwa Kenya na Uganda, hivyo kuvunjika kwa University of East Africa na kuanzishwa kwa vyuo vya Makerere University, University of Nairobi, na University of Dar es Salaam. Chuo kikuu cha Dar es Salaama unachojua leo kilianzishwa rasmi kwa sheria ya Bunge namba 12 of 1970 baada ya kuvunjika kwa University of East Africa.
 
Wana JF nani ana hii Historia ya kuanza hiki cha ya Mlimani (UDSM)

Sent using Jamii Forums mobile app

Dossa Aziz na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Ilikuwa kawaida ya Dossa baada ya mikutano ya TANU pale Mnazi Mmoja kumchukua Nyerere na gari lake kumrudisha Pugu. Njia ya zamani kwenda Pugu ilikuwa inapita hapo kilipo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Sasa ilikuwa kiza kimeingia na walitaka kutoka nje ya gari kuangalia mandhari ya Dar es Salaam maana kutokea pale mji ulikuwa unapendeza sana kwa taa zilizokuwa zikiwaka barabarani. Nyerere alimwambia Dossa, “Dossa tukipata uhuru wetu hapa lazima tujenge chuo kikuu.” Hili wazo lilifanyiwa kazi na wananchi wakahamasishwa kuchangia ujenzi wa Chuo hicho. Fedha zilichangwa na Chuo kikajengwa pale New Street kwenye kiwanja cha John Rupia alichokitoa kuwapa TANU. Hapo ndipo kilipoanza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. (Chuo hiki sasa ni Chuo Cha Watu Wazima). Abdallah Salum alikuwa mmoja wa wachangiaji wa chuo hicho na mwanae Salum Matimbwa hadi leo amehifadhi stakabadhi ya malipo ya sh. 50.00 stakabadhi ambayo ina sahihi ya Bhoke Munanka. Wazee hawa walikuwa wazalendo wa kweli kabisa.
 
Here comes Mzee Said

Kwenye eneo hili la ubora wako hauna mpinzani
 
Here comes Mzee Said

Kwenye eneo hili la ubora wako hauna mpinzani
Pinno,
Hii ni historia ya wazee wangu katika kutafuta maendeleo ya watu wa Tanganyika.

Nakuwekea hapo chini baadhi ya majina ya watu waliochangia ujenzi wa Chuo Kikuu
Cha Dar es Salaam:

Mr. Salun Athumani
  • Mr. D.P.K. Makwaia
  • ,J.K. Nyerere
  • .s.
    Mr. Juma Mzee

    Mr.Ibrahim Bofu
    • Mr. Schencider Plantan
    • Mr. Abdallah Said
  • Mr. Athman A'rahaman
    • · Jayanti Stores l0. Alli Chance
    • Mr.Kondo Salum
  • Mr.Athaman Aman
    • Mr. Lucas Musungwa
    • Mahadi Mwinyijuma
    • Mr. Abbas Skyes
    • Makatta mtwana
    • Mr. Elias Millinga
    • Mr. Abbas Max
    • Mr. Salum Athuman 20. Mr. Korongo Juma
  • Mr. Alli Mohamed
    • Mr. Mohamed Sefu
    • Messrs Thank.en
  • Mr. Hamis Hassan
    • Mr. Hamis Tambwe
    • Mr. Sultan Dibega ·
  • Mr. Yusufu Abdallah
    28. Mr. Msibu Selemani
    • Mr. Rajabu Athwnan
  • Mr. Alli Abdallah
    • Mr. Mohamed Mukande \
    • Mr. Husein Kahurnu
  • Mr. Mrisho Bilali
    • Mr. Francis Kashaija
    • Mr. ldi Faiz Mafongo
    • Mr. Max Bwana
    • Mr. Y. Max
  • Mr. Alli M. Haloua
    • Mr. Has.sam Mukhosini
  • . 40. Mr. Amlor!1!JUS
    U. Mr. Bakan Mzee
    n. Mr. Saidi Salimu
    • Mr. Mgeni Saidi
  • Mr. Swalehe Abdallah
    • Mr. Mzce Mwinytchande
    • .Mr. Sharia Bofu ·
    • Mr. Khalili Marjani
    • .Mr. Salimu Kambi
    • .Mr. Abdallah Salimu
  • 50. .Mr. JumanneSuleman
    • .Mr. Bibi Tuhunia Dauli Kirumbi
    • Mr. Hadji Yakuru
  • . 5 3. .Mr. Costa Albert
    I
    Mr. R. Machado Plantan
    • Mr. Salurn Hanusi
  • Mr. Maneno KilongoI1l
    57.·Mr. Ferdinand Basimaki
    58. Mr. Nicholas Kuhanga
    59. Mr. J. Mohamed Rashid
    Mr. Zayyid Hamisi
    • l
      Mr. Alli Said
      • Bibi Mariam Madengc
    • 64. Mr. Abubakari Alli
      50.00
      50.00​
      65. Mr. Abjed Fundi
      50.00​
      66. Mr. Moh.amed Omari
      50.00​
      67. Mr. Salim Mlapakoro
      50.00​
      68. Mr. M.S. Shinene Durry
      50,00'​
      69. Mr. Isidore Kulunga
      50.00​
      10. Mr. Pius Makuwege
      50.00​
      71. Mr. Alimasi Sefu
      (l.00​
      12. Mr. Lila Mwinyikondo
      50.00​
      73. Bibi Panya Majaliwa
      50.00​
      74. Mr. Abdallah Simba
      50.00​
      3. Mr.F. V. Mponji

      D'Salaam

      Pugu College

      Tanga Boundary Iringa

      Pugu College

      I
      500.00
      S00.00
      200.00
      150.00
      150.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      100.00
      50.00
      ·50.00
      .50.00
      50.00
      50.00
      5so0..o0o0​
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      . 50.00​
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      5G.OO
      50.00
      50.00 50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      0.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00
      50.00 . 50.00 50.00

l

.
 
Dossa Aziz na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Ilikuwa kawaida ya Dossa baada ya mikutano ya TANU pale Mnazi Mmoja kumchukua Nyerere na gari lake kumrudisha Pugu. Njia ya zamani kwenda Pugu ilikuwa inapita hapo kilipo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Sasa ilikuwa kiza kimeingia na walitaka kutoka nje ya gari kuangalia mandhari ya Dar es Salaam maana kutokea pale mji ulikuwa unapendeza sana kwa taa zilizokuwa zikiwaka barabarani. Nyerere alimwambia Dossa, “Dossa tukipata uhuru wetu hapa lazima tujenge chuo kikuu.” Hili wazo lilifanyiwa kazi na wananchi wakahamasishwa kuchangia ujenzi wa Chuo hicho. Fedha zilichangwa na Chuo kikajengwa pale New Street kwenye kiwanja cha John Rupia alichokitoa kuwapa TANU. Hapo ndipo kilipoanza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. (Chuo hiki sasa ni Chuo Cha Watu Wazima). Abdallah Salum alikuwa mmoja wa wachangiaji wa chuo hicho na mwanae Salum Matimbwa hadi leo amehifadhi stakabadhi ya malipo ya sh. 50.00 stakabadhi ambayo ina sahihi ya Bhoke Munanka. Wazee hawa walikuwa wazalendo wa kweli kabisa.
A bunch of stuff!!
 
Back
Top Bottom