Mwenye kujua tofauti ya mfanyabiashara na mjasiriamali.

BJBM

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2011
Posts
664
Reaction score
600
Habari zenu wakuu. Natumai nyote ni wazima.
Kama mada tajwa hapo juu inavyojieleza, ningependa kujua tofauti kati ya watu hao wawili kwani nimekuwa nikipata shida sana katika kutofautisha kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara.
Uzi huu nimeufungulia jukwaa hili nikiamini ntapewa majibu kwa ufasaha zaidi.
Naomba kuwasilisha.
 
Mfanyabiashara ni mtu yeyote anayefanya biashara iwe kubwa au ndogo.

Mjasiriamali ni mtu mwenye kuamini mawazo yako, malengo yake na ndoto zake katika shughuli fulani ya kujiajiri mwenyewe inaweza kuwa biashara au isiwe biashara.

Mfano mtu anaweza kuwa na ndoto ya kujiajiri kwa kufundisha, kusafisha mitaro nakadhalika.

Kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara lakin si kila mtu anaweza kuwa mjasiriamali sababu ujasiriamali ni zahidi ya biashara.

Mjasiriamali anatakiwa ajitambue na awe na mikakati ikiwezekana ajifunze shughuli anayotaka kujiajiri kabla ajajiajiri.

Haya swali lingine ...
 
Asante mkuu kwa kunielewesha. Nimekuelewa lakini in a very thin line, nahitaji nikuulize zaid ili nami nipanuke kiuelewa katika hili.
Umesema,"Mjasiriamali ni mtu mwenye kuamini
mawazo yako, malengo yake na ndoto
zake katika shughuli fulani ya
kujiajiri". Unataka kuniambia wafanyabiashara asilimia kubwa wanakuwa hawana malengo, mawazo wala ndoto zakufikia ktk kile wanachokifanya?
 
Hii mada yako ungepeleka jukwaa la biashara ungepata majibu mazuri.

Ili jukwaa la elimu wamezoea kubishana gpa hakina mpiga msuri na sayansi kimu ndio maana unaona limekosa wachangiaji.

Mada za biashara zipelekwe jukwaa la biashara ndio kuna majibu mazuri.ili jukwaa la elimu halina tofauti na siasa
 
Mjasiria mali ni yule anayeangalia fursa katika eneo husika na kutumia ile fursa ambayo wengine hawakuweza kuitumia kujiingizia faida iwe katika biashara au hata ujuzi wowote ule mtu anaweza kuwa mjasilia mali....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…