Mwenye kulijua hili shirika linaloitwa "SAFAYA" anijuze tafadhali

Kamyamya

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
560
Reaction score
572
Kuna jamaa yangu mmoja kanipigia simu asubuhi ya leo akiwa Mwanza akinitaka nijiunge na hili shirika kwa ahadi ya kunufaika kiuchumi baada ya kushiriki mafunzo yao na kutoa kiingilio cha Tz shs 100,000.

Niwaombe wakuu wangu humu jamvini kabla sijaingia chaka mnipe uzoefu wa hawa jamaa.
 

Amekuambia ni mafunzo gani?

Utanufaikaje kiuchumi?

Ni pyramid scheme kama akina Kalynda ambako unaweka hela tu halafu kiajabu hela zinajizaa na kuongezeka bila uzalishaji wo wote?

Sema mafunzo ambayo ndugu yako alipewa. Na kama huo unufaikaji wa kiuchumi unazingatia misingi ya taaluma ya Uchumi na siyo chuma ulete!
 
Siku hizi Kuna wengine wanajiita bombastic angency eti kiingilio 13000 unapata mpaka laki kwa siku
Utapeli mtupu tu
 
Na serikali wanachekelea hizi schemes kwasababu wanamgao wao pale wanainchi wakishapigwa mabilioni ya pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…