Mwenye kumbukumbu ya maneno yaliyotumiwa na CCM kwenye uchaguzi mkuu2005 ayaweke hapa

Mwenye kumbukumbu ya maneno yaliyotumiwa na CCM kwenye uchaguzi mkuu2005 ayaweke hapa

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
2,364
Reaction score
867
Waungwana wasalaam?

nakumbuka mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mkuu viongozi wa ccm waliopo madarakani sasa walitumia maneno na majina ya ajabu kwa wagombe wenza hasa wa vyama vya upinzani mfano mkoa wa Tabora,Mwanza,na Shinyanga,kulikuwa na maelekzo toka kwa wapiga debe wa ccm kuwa katika majina matatu ya wagombea wa urais ongeza VU na kama likileta maana basi usimchague huyo mtu kuwa Rais nalisipoleta maana huyo mtu anafaa kuwa Rais wa Tanzania



Mfano:

MREMA+VU=

LIPUMBA+VU=

KIKWETE+VU=hili halikuleta maana na ndiyo maana leo ni Rais wa JMT,na kama mnavyojua mtaji wa ccm uko sana mikoa hyo na watu wa mkoa ya kanda ya ziwa kielimu wako chini sana na wepesi wakuamini maneno ya uongo na bila kuyatafakali,japo kwa sasa wamechange kutokana na elimu ya uraia inayotolewa na M4C+Asasi za Kiraia


RAI YANGU:

haya maneno naomba yasitumiwa tena kwenye uchaguzi mkuu ujao na wala vyama vya upinzani visitumie maneno kama hayo ya kudharirisha utu wa mtu kisa madaraka.


kwa wenzangu wa mikoa ya arusha,mtwara.iringa.mbeya,dodoma,kulikuwa na maneno gani kwenu huko mwaka 2005? hata 2010 ili tuombe hayo maneno yasijirudie tena na tena
 
''RAI YANGU:

haya maneno naomba yasitumiwa tena kwenye uchaguzi mkuu ujao na wala vyama vya upinzani visitumie maneno kama hayo ya kudharirisha utu wa mtu kisa madaraka.''

Unaonaje uki balance ishu hapa yaani utaje pia vyama vingine vilitumia maneno gani pi!! ni mawazo yangu tu!!!


kwa wenzangu wa mikoa ya arusha,mtwara.iringa.mbeya,dodoma,kulikuwa na maneno gani kwenu huko mwaka 2005? hata 2010 ili tuombe hayo maneno yasijirudie tena na tena[/QUOTE]
 
jogoo linawika....CCM inawenyewe.....CCM iendelee kuyatumia, yana MAANA HALISI, nikweli inawenyewe...MAFISADI....
 
Mbona simuoni mbowe. Maana alipeperusha tiketi ya cdm. AHADI YA CCM! NITAWAPA MAHAKAMA YA KADHI HUKU AKIJUA HAIWEZEKANI. NA NDIO CHANZO CHA VURUGU ZA KIDINI.
 
ndiyo maana nimetoa wingo mpana zaidi.......mie nilickia upande wa ccm tu na kama na ww ulikuwepo pls weka upande wa pili wa shilingi
 
Nimeomba hayo maneno tusiendelee kuyatumia mandieta pls
 
Maisha bora kwa kila mtanzania! Sasa sijui kwa nini hii kauli mbiu haikutumika 2010! Karibuni tudadavue Kwa nini hii kaulimbiu haikurudiwa tena?
 
Mbona simuoni mbowe. Maana alipeperusha tiketi ya cdm. AHADI YA CCM! NITAWAPA MAHAKAMA YA KADHI HUKU AKIJUA HAIWEZEKANI. NA NDIO CHANZO CHA VURUGU ZA KIDINI.
Hebu tulia uandike vizuri. Mbowe alisema atawapa waislamu mahakama ya kadhi au CCM walisema watatoa mahakama ya kadhi?

HATA HIVYO

CCM waliidandia hii hoja haikua yakwao. Mhe. Lyatonga Mrema Augustine ndiye alilipenyeza hili wakati yupo TLP, Kama nakumbuka vizuri ilikua mkoani Morogoro, CCM wakaona huyu mzee anaondoka na waislamu wote kwakua hicho kilikua na Ni kilio chao cha muda mrefu sana.
 
Back
Top Bottom