Ulipendapo waridi
Jali wake uchungu
Uchunguze muwaridi
Miba mingine michungu
Ukilitaka waridi
Chagua lilo stadi
Usilipende waridi
si rangi ilimradi
Ukilipenda waridi
Chagua lisokaidi
Ukilipenda waridi
Si lazima likuzidi
Ukilipenda waridi, changua likufaalo.
Mi mwenyewe nimejifunza kuipenda na jinsi ya kukaa na miba yake, maana niligundua hata mie nina miba yangu ,ila aishie na mimi hana budi kuipenda ili isimchome
Mi mwenyewe nimejifunza kuipenda na jinsi ya kukaa na miba yake, maana niligundua hata mie nina miba yangu ,ila aishie na mimi hana budi kuipenda ili isimchome