Mwenye nguvu amkaa! mwenye weledi changamka wewe!

Mwenye nguvu amkaa! mwenye weledi changamka wewe!

Kiulajere

New Member
Joined
Feb 18, 2025
Posts
1
Reaction score
3
Mwenye nguvu amkaa! mwenye weledi changamka wewe!... shida nini? .

Tunataka nchi isonge mbele, tunataka tufanane na mataifa makubwa ya Ulaya , tuwe na miundombinu ya kisasa kama viwanja bora vya ndege, barabara nyingi za kupunguza msonganano, Vituo bora vya afya na nambo mengi ya kileo.

Lakini ndiyo kwanza tunajipanga kila siku nakautekelezaji cha viwango fulani hivii! . Sifa kibao za wewe nchi yangu " nikienda mbali nawewe " unasifika huko wewe acha tuu!, una madini ya kipekee lakini watoto wako hata rangi ya madini hayo hawaijui, una mbuga nzuri za wanyama "watoto wako wengine wanaishia kusimuliwa na kutazama kwenye runinga" .

Wataalamu wachanga (wenye uzoefu mdogo wapo mtaani ) nchi yangu unadai " Wajiajiri " mbona wewe unakopa nje? , wewe nchi yangu na wataalamu wengineunaosema unawazalisha zipo wapi taaluma zao Kama lazima uwapitishe kwenye usaili kwani hauamini taasisi ulizo ziweka mwenyewe kuzalisha wajenzi wa taifa?

Kwani zinazalisha nini sasa? Na je? hawakupita usaili wako unawatupa wapi?. Amka nchi yangu !!
 
Back
Top Bottom