Mara nyingi maneno haya mawili yanataja watu walewale lakini inawezekana kuna tofauti. Mtazamo ni tofauti.
"Raia" inaangalia upande wa kisheria: je mtu fulani anatosheleza masharti ya kuitwa "raia" wa nchi fulani, pamoja na haki (kama kura, haki ya kusikilizwa na kulalamika, kutetewa na ubalozi wake akiwa ugenini) na wajibu (kwa mfano kwenda jeshini katika nchi nyingi, kushiriki katika wajibu fulani) za uraia.
"Mwananachi" inatazama zaidi tabia ya kuishi (kwa muda usio mfupi) katika nchi au sehemu fulani, kuwa mwenyeji wa huko.
Kwa kawaida hakuna utaratibu wa kisheria au masharti kamili ni nani anayeweza kuitwa "mwananchi", tofauti na "raia".
Unaweza kuishi katika nchi nyingine hadi umekuwa mwenyeji na kila mtu anakutazama kuwa mwananchi lakini bado hujafanya hatua ya kuomba uraia.
Mara nyingi tofauti hii si tatizo lakini kutegemeana na siasa ya nchi fulani tatizo linaweza kutokea.
Kwa mfano huko Marekani Bwana Trump anajaribu kuwaondoa watu waliokuwa wenyeji kwa muda mrefu hata kizazi cha pili kwa sababu zamani waliingia kutoka Meksiko, si raia.
Nakumbuka majadiliano sawa kuhusu Banamulenge nchini Kongo waliokuwa wenyeji na wananchi kwa vizazi lakini walinyimwa uraia na kutangazwa kuwa Warwanda kwa sababu za ukabila na siasa.