Mwenye uelewa anisaidie tofauti ya raia na Mwananchi

Mwananchi ni kama wewe, raia wanatofautiana kuna raia vilaza na raia mtu
 
Raia anatokana na mwananchi/wananchi, mfano wanachi mkoani Mbeya wamejiandikisha katika daftari la wapiga kura kujiandaa na uchaguzi wa mwaka huu. Lkn katika zoezi hill kumetokea na dosari kadhaa ikiwa ni pamoja na kuandikishwa kwa wananchi wasio na sifa za uraia. Mfano wa pili ni wakimaeneo kuna makazi ya kijeshi kama vile polisi, magereza,jwtz nk, haya tunaita makazi ya majeshi, lkn maeneo kama vile Manzese, mwanjelwa, magomeni, soweto, haya tunayaita makaazi ya raia lkn wote ni wananchi wa sehemu hizo
 
Naongezea juu ya maelezo ya wenzangu. Mwananchi ni mtu anayeishi katika nchi; ni mwenyeji wa nchi kijamii na kimakazi. RAIA ni mwenyeji wa nchi kisheria na kisiasa. Ana haki ya kushiriki maamuzi na matendo rasmi ya kisheria na kisiasa. Zingatia kwamba, mwananchi anaitwa hivyo sababu anaishi nchini, Ila RAIA in RAIA kwa belonging hata kama haishi nchini
 
Hayo in matumizi ya lugha ya kimtaani au matumizi mengine ya neno RAIA. Lakini, kwa maana yenyewe, hats mwanajeshi in RAIA was nchi
 
raia - wote ambao sio askari

mwananchi - wote (askari na raia)
 
Mimi nadha ni kiswahili ni shida..

Uraia inabeba dhana ya utaifa wa mtu
Mwana+nchi inabeba dhana ya mzawa wa eneo husika maana yake raia ambaye ni mzawa wa nchi husika au sehem husika.....

Sasa linapokuka Suala la askar amengia uraiani
Wanachi wapgana na askari
Wanajeshi wapigana na raia
Hapo sasa ufafanuz wake ndo utata...
 
yote yana maana sawa ila yanatumika katika muktadha tofauti...hiyo ni kawaida katika lugha kuwa na visawe ktk lugha,
kwa mfano maneno angalia, tazama, ona yanamaana sawa but huwezi sema nilikuwa naona mpira bali utasema nilikuwa natazama mpira
 
Mkuu wapo wengi na wengine wametlelkezwa kwenye kambi huko ALASKA !!
Unachosema ni kweli kulingana na Historical Theories. Lakini kiuhalisia dunia hakuna binadamu mwenye asili hiyo. Historical Theories nyingi zimewapoteza watu wengi wenye elimu ndogo ya Historia. Mfano ni ile Dawning Theory inayosema binadamu wa kwanza wa Afrika alikuwa sokwe/nyani. Kwa mtu mwenye elimu Histori ya form four na six ataendelea kuelewa hivyo.
 
naomba nichangie kidogo,neno raia katika asili yake ya kiarabu lina maana ya watu wanaoongozwa,kwao wana neno rai ni kiongozi na raia waongozwa.
mwananchi ni muhusika wa nchi fulani bila ya kujali kama ni kiongozi au kiongozwa.
rai kikwete alizoea kusema"NDUGU WANANCHI WENZANGU" NA sio raia wenzangu
 
Kwa kuanza niseme lugha ya kiswahili ina namna zaidi ya kumi za uundaji wa maneno. Neno mwananchi liliundwa katika muundo ambatano yaani. Mwana lina maana mzawa au mtoto na neno Nchi linamaana eneo la kimpaka la taifa fulani, maneno haya ukiyachunguza yalitokana na shughuli za kisiasa.

Neno RAIA ni neno lenye maana ya ukaazi mtu wa nchi fulani kisheria
Jamani huwa nashndwa kujua au kutofautisha kti ya neno RAIA na MWANANCHI.Hebu nipeni ufafanunuzi.
 
yote yana maana sawa ila yanatumika katika muktadha tofauti...hiyo ni kawaida katika lugha kuwa na visawe ktk lugha,
kwa mfano maneno angalia, tazama, ona yanamaana sawa but huwezi sema nilikuwa naona mpira bali utasema nilikuwa natazama mpira
Naangalia
 
Asante kwa elimu wakuu kama bado mpo jamiiforums.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…