Frequency ni marudio ya hatua/mapigo/mzunguko fulani kwa sekunde.
Mfano ni tairi la baiskeli linapofanya mzunguko mmoja kwa sekunde, hiyo ni sawa na frequency mmoja. Frequency inatumia kipimo cha hertz (Hz). Kadiri tairi linavyozunguka haraka frequency nayo inaongezeka, ikimaanisha litazunguka mara nyingi katika sekunde ile ile moja.
Mwanga wa jua pia unatoa frequencies nyingi ila tunaotambua sisi binadamu ni huo mwanga wa rangi saba ( zile za upinde wa mvua).
Wakati tsunami ile ya kule mashariki ya mbali ilipotokea, wanyama wote kama mbwa na paka walikimbilia sehemu zenye miinuko, dakika 30 kabla ya wimbi la kwanza kuja. Wao waliweza kusikia frequency za hilo wimbi ila binadamu hawakuweza.
Viumbe hai mbalimbali wanauwezo tofauti wa kutambua frequencies mbalimbali. Mfano binadamu wanauwezo wa kusikia sauti kati ya frequency ya 20Hz na 20KHz, nje ya hapo binadamu hawezi kusikia. Mbwa kwa upande mwingine anaweza kusikia sauti zaidi ya 20kH.
Hata inapokuja kwenye kuona kuna frequencies chache sana ambazo binadanu wanauwezo wa kuona (visible light) nje ya hapo hatuoni. Mfano kwenye giza totoro, binadamu anakuwa kipofu ila kuna baadhi ya wanyama , kama nyoka, wanaweza kuona vizuri tuu usiku. Hii ni kwasababu wanauwezo wa kutambua lower frequencies kama infra red.
Kuhusu hivyo viumbe vinavyoweza kutuona, kama kweli, vipo basi vitakuwa vinaweza kutambua ranges nyingi za frequencies kuliko sisi.