Unakubaliana nae kwa lipi? Kama hamjui Spare Parts kuagiza ni rahisi kuliko gari maana hata kuchelewa kwake huwa haizidi wiki mbili!Nakubaliana na wewe kiongozi.
Hizo wiki mbili unazosubiri shughuli zako za hilo gari zitakuwa zimekwama.Umewahi kuagiza Spare Parts? Kipi Gharama, kuagiza spare halisi ambayo utaipata ndani ya wiki moja au mbili au kwenda kununua spare feki ya Toyota? Hizo spare mnazosema ni rahisi kupatikana nyingi ni feki au used ambazo uimara wake ni wa kubabaisha sanaaa.
Tatizo kubwa wabongo wengi ni waoga sana wa vitu vidogo vidogo. Mtu unaagiza gari unalisubiria miezi miwili ila unaogopa kuagiza Spare Parts!
Inategemea umeagiza wapi...alafu kumbuka magari mengi mnayoendesha bongo ni ya zamani na used, na hata yalipotengenezwa hayakutengenezwa kwa ajili ya soko letu hivyo kama unajua mambo ya magari na spare parts utanielewa ninachosema. Pia unapokuwa na gari sio jambo la ajabu kupaki gari kwa wiki moja au mbili kusubiria spare uliyoagiza. Mfano Befoward wanauza spare na kampuni nyingine kibao tuu.Hizo wiki mbili unazosubiri shughuli zako za hilo gari zitakuwa zimekwama.
Ni tofauti na mtu anateenda kununua spare inayopatikana dukani.
Halafu si kweli kuwa spare zote zinazouzwa kwenye maduka nchini ni feki.
Vilevile kumbuka kuwa unapoagiza kitu, sio lazima uletewe kilekile ulichotarajia.
Ndio maana tunachofanya ni comparison.Inategemea umeagiza wapi...alafu kumbuka magari mengi mnayoendesha bongo ni ya zamani na used, na hata yalipotengenezwa hayakutengenezwa kwa ajili ya soko letu hivyo kama unajua mambo ya magari na spare parts utanielewa ninachosema. Pia unapokuwa na gari sio jambo la ajabu kupaki gari kwa wiki moja au mbili kusubiria spare uliyoagiza. Mfano Befoward wanauza spare na kampuni nyingine kibao tuu.
Ndio maana tunachofanya ni comparison.
Gari A unasubiri spare wiki mbili, gari B unaenda kununua spare straight dukani.
Gari la bei ndogo kama Mazda Demio, kuagiza spare nje ni kujitia gharama zisizo na umuhimu. Gari ya mil 8 unaagiza spare sh laki 6 ambayo kwa gari nyingine kama Toyota ungepata dukani kwa sh laki 2.
Asante mtani wangu, nimepiga kambi hapa kitambo Sana.Karibu tujifunze wote mtani.
Asante kiongozi.Kiongozi asikwambie mtu nimemiliki hii gari kwa miaka minne kabla ya kuuiza kwa jamaa yangu ambaye mpaka sasa ni mwaka wa nne naye akiitumia. Nilikiuza kwa sababu nili upgrade kwenye gari kubwa zaidi!
Ni gari yenye roho ya paka, nimekuwa na routes za Dar-Dom kila mwezi kwa miaka 4 na bado haikuleta shida. Niliwahi gonga chini nikakata chuma kinachounganisha tyres 2 za mbele (jina sikumbuki) bei yake ilikuwa laki nne. Ila baada ya kufunga ni mkataba. Kiko imara barabarani, fuel economy, binafsi kilikuwa kinakwenda mpaka 19km/litre of petrol. Japo ni kidogo kwa nje, ndani Kina nafasi ya kutosha, kama vipi ukilaza ile siti ya nyuma ile buti ni kubwa sana kuweka mizigo.
Vitu vya msingi:
1. Kiinue kabla hujaanza kukisulubu kwenye barabara zetu
2. Epuka kubeba mzigo mzito kuliko uwezo wa gari
3. Hakitaki mashindano speed ukienda sana 120km/hr
Mwisho kama wewe ni dereva mzuri inakopita Bajaj na wewe waweza pita na Mazda!!
Kila la heri!
Rapid nafikiri jamaa walikuibia.Nilikuwa na Mazda demio,inatumia mafuta kidogo sana kilomita 15 kwa 1lita.Vifaa vyake vipo juu sana.Kwa mfano shock up za nyuma tu zinauzwa 960,000/=
Kagumu sana,kenye cc1500 kanatembea kweli,Mazda Demio ni gari ngumu binafsi ninaimiliki na nimekuwa nayo kwa miaka minne iko poa sijawahi badilli kitu likubwa zaidi ya shockup na engine mounting,ulaji WA mafuta ni mzuri,body yake ngumu sana hasa model za 2000 mpaka 2004 na hivi sasa nimeiweka sokoni ninaiuza kwa atakaevutiwa nayo anipm bei milioni 4 tu kwakuwa nimeshaitumia naamini ni fair price.
mkuu upo sahihi sana harafu wabongo ni wepesi sana wakulumu mfano mzuri spare za nissan wanasema ni ghali lakini sio kweli ughali unawekwa na mafundi na wauzaji wetu wa spare hapa bongo ukitaka uone vituko nenda ilala katafute spare ya nissan harafu wakati huo huo ingia mtandaoni angalia bei yake kuagiza mpaka hapa bongo uone utofauti mkubwa.Umewahi kuagiza Spare Parts? Kipi Gharama, kuagiza spare halisi ambayo utaipata ndani ya wiki moja au mbili au kwenda kununua spare feki ya Toyota? Hizo spare mnazosema ni rahisi kupatikana nyingi ni feki au used ambazo uimara wake ni wa kubabaisha sanaaa.
Tatizo kubwa wabongo wengi ni waoga sana wa vitu vidogo vidogo. Mtu unaagiza gari unalisubiria miezi miwili ila unaogopa kuagiza Spare Parts!
Na cha ajabu hizo gari ni bei rahisi. Sijui zinakua labda Zina shida yyte labda.mimi naikubali sana hii gari mazda tribute hata nikikutana nayo humo barabarani lazima nisimame kuiangalia vipi kuhusu hii
Naomba mwenye kujua vizuri haya magari, hasa model za 2004 kurudi nyuma. Uzoefu wa spare parts, fuel consumption, kuhimili mikiki ya njia zetu nk.View attachment 373742View attachment 373743View attachment 373744