Mwenye ujuzi wa biashara ya Chapati kwa kutumia majiko makubwa

Nguvu sio Pesa

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2013
Posts
380
Reaction score
284
Wakuu,
Poleni Na majukumu.Rejea kichwa cha habari hapo juu.
Mwenye uzoefu wowote Wa biashara amwage nondo hapa tuweze kujifunza hii baishara.

Nimeona majiko mawili makubwa maeneo ya kimara stendi.".vijana wako bizy" sana wanachoma chapati Na inavyonekana wanapata wateja wengi sana..wanaotoka makazini wanaoenda kazini shift za usiku.

Majiko niliyo yaona ni ya kuchoma chapati sita kwa mpigo.Nilijaribu kuuliza vijana wale lakini hawakua open kwangu kivile.
 
Hiyo biashara ndio kama "habari ya mujini" kwa sasa,.ww ulikuwa unataka kuijua kwa kutaka kuifanya,au unataka kujua upatikanaji wa hilo jiko au kujua tuu uendeshaji wa biashara hii na gharama,faida pamoja na changamoto zake???
 
Hiyo biashara ndio kama "habari ya mujini" kwa sasa,.ww ulikuwa unataka kuijua kwa kutaka kuifanya,au unataka kujua upatikanaji wa hilo jiko au kujua tuu uendeshaji wa biashara hii na gharama,faida pamoja na changamoto zake???
Mkuu nahiyaji kujua gharama ya uendeshaji changamoto zake pamoja Na faida?nataka nifanye huku Geita Katoro.
 
Ndugu, hongera kwa kuwaza maendeleo.
Hiyo biashara ni nzuri. Biashara ya chapati inalipa sana kama utapata eneo lenye wateja wengi.
Chapati hutofautiana bei kulingana na maeneo na ubora, wapo wanauza 350, 400, 500 had 1000.
Kwa kawaida hata tunapopika majumbani unga nusu utoa chapati 6 na kilo 12 au 11 kulingana na ukataji.
Bei za unga hutofautiana kulingana na maeneo na aina ya unga. Mfano, ukinunua unga kg 1@1500 mafuta robo 1000 mkaa 1000 =3500 jumla ukauza chapati 12×500=6000 faida yako itakuwa 2500. Kama utapika kilo 10 maana una 25000 kwa siku.
Kuhusu vifaa. Panahitajika jiko kubwa na meza ya kusukumia(sio vibao vya chapati). Maana unaweza kuta mtu katandika chapati hata kumi mezani anasukuma kwa speed.
Kwa geita ulikosema sijui wanapouza majiko na kikaango, ila kwa dar kkoo ni mengi.

Kuhusu mtaji, inategemea wingi wa wateja. Kuna mama wakati nasoma nilikuwa nakula kwake chapati, kaajiri kijana anakanda kg 25 kila jioni anauza na maharage zinaisha.

Changamoto zipo kama ilivyo kwenye biashara nyingine, kuna kukosa wateja nk. Kazi ya kukanda kupika inaumiza kifua sana.
 
Good response mkuu
 
mkuu asante sana kwa hizi Nondo.Ubarikiwe sana ubarikiwe sana......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…