Mwenye utaalam huu wa kuku wa kienyeji

Mwenye utaalam huu wa kuku wa kienyeji

Manselly

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
456
Reaction score
130
jamani mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji ila kila napototolesha vifaranga majogoo wanatotolewa wengi kuliko matetea.
Naomba kujuzwa kama kuna tecknolojia ya kulitambua yai lenye kifaranga cha kike au cha kiume kabla ya kutotolesha.
Najua hapa wataalam wapo wengi hebu nipeni mbinu
 
Kuna tochi kama ya kumulikia masikioni wanayotumia madaktari nenda kanunuwe pale sabasaba kwenye maonesho ya nanenane. Maelekezo watakupa namna ya kutumia.
 
Nenda jukwaa la ujasiriamali watakusaidia mkuu
 
Kuna tochi kama ya kumulikia masikioni wanayotumia madaktari nenda kanunuwe pale sabasaba kwenye maonesho ya nanenane. Maelekezo watakupa namna ya kutumia.

shukrani sana japo ungekua unafaham jina la hicho kifaa ingekua poa sana
 
Kuna tochi kama ya kumulikia masikioni wanayotumia madaktari nenda kanunuwe pale sabasaba kwenye maonesho ya nanenane. Maelekezo watakupa namna ya kutumia.

Nadhani kazi ya ile tochi ni kukuonyesha kwamba Yai lina uzazi ama haliwezi kuwa na kifaranga, lakini sio la kuonyesha kuwa ni jogoo ama tetea

niliwahi kusikia watu wanatambua kwa kuangalia shape ya Yai tu,
 
Yai lililochongoka sana kichwani ni jogoo....ambalo halijachongoka sana ni tetea....ndivyo nilivyokariri.
 
Kuna mtu alinijuza kuwa mayai yaliyochongoka zaidi ni majogoo..hivyo wakati wa kuatamisha kuku tumia zaid yaliyo duara.. bado sijafanyia hili kazi kupata uhakika.
 
Nadhani kazi ya ile tochi ni kukuonyesha kwamba Yai lina uzazi ama haliwezi kuwa na kifaranga, lakini sio la kuonyesha kuwa ni jogoo ama tetea

niliwahi kusikia watu wanatambua kwa kuangalia shape ya Yai tu,
Kisichowezekana kwa mwafrika kwa Mzungu kinawezekana.
 
Yai lililochongoka sana kichwani ni jogoo....ambalo halijachongoka sana ni tetea....ndivyo nilivyokariri.
Haswaaaaaa. La jogooo huwa kubwa la tembe huwa dogo na la koroa huwa kubwa ila halijachongoka.
 
Hii njia sio kweli ni sawa na kupiga Lamuri, Kuna Kuku wanataga mayai yaliyoChongoka tu na yakitotolewa unakuta mchanganyiko, so sio kweli, Hakuna njia ya kuweza kufanikisha hili
 
Kama unatumia kiatamizi joto lake lipo juu kuliko linavyostahili.
 
nashawishika kukubaliana nawe, hii kitu niliisikia miaka mingi, muulizaji kama anatumia kiatamizi ajaribu ku-adjust joto
 
Back
Top Bottom