Mwenye uzoefu na biashara ya Dry cleaner anijuze

kimara Kimara

Senior Member
Joined
Jul 7, 2024
Posts
141
Reaction score
287
Habari za muda Huu wadau, Mwenye uzoefu au anayefanya biashara ya Dry cleaner anijuze.

Changamoto za biashara iyo

Faida za biashara

Soko linapatikana vipi (wateja)

nakadhalika...

Asante..
 
Habari za muda Huu wadau, Mwenye uzoefu au anayefanya biashara ya Dry cleaner anijuze.

Changamoto za biashara iyo

Faida za biashara

Soko linapatikana vipi (wateja)

nakadhalika...

Asante..
Mtaji Laki 7 tu unatosha
Vifaa muhimu
Machine ya kufulia 1 au 2
Machine ya kg 9 inauzwa 530,000/=
Kama budget yako ndogo Anza hata na machine moja mwanzo mgumu.
Bei za kufua
Shati/t-shirt 1000
Suruali 1500
Makoti 2000 mpaka 3000
Blanket 5000
Mashuka 2000
Duvet 10000
Viatu 2000

Matenga
Tenga 1 = 13000
Nusu Tenga 7000

Gharama za kila siku
Sabuni kg 5 = 12000
Maji = 1000
Jumla ya gharama za kila siku 13000
Wastani wa mapato na FAIDA kwa siku
Mfano ukipata wateja wa Tenga 4 kwa siku
4*13000 = 52000
FAIDA ya siku
Mapato=52000-13000
FAIDA kwa siku 39000🔥

Mambo ya kuzingatia
1. Tangaza biashara yako kila siku
2. Toa vipeperushi (flyers)
3. Usianze na bei kubwa sana
4. Usikatae hela (mteja ni mteja)
5. Kuwa msafi na mwaminifu hii ndo siri ya kupata wateja wa kudumu.
 
Huu uzoefu wa kuuliza Jamii? Mnacheza na mitaji nyinyi ya Biashara
 
Tafuta location lakini lodge na hotel za karibu ambazo hazina huduma za kufua au zinategemea wafuaji wa mikono wote ni wateja wako, usishahu commision,kila nguo ya mteja wa lodge meneja apate percent
 
Hii kauli ya 'huwezi nielewa' ni kauli isiyo na msaada wowote siku zote
Alafu kauli kama hiyo inatumikaje kwenye biashara? Mwenye Uzi anahitaji maelezo ya biashara Lakini Cha kusikitisha watu wanajibu kwa mkato.
 
Dry cleaner,hivi wanakaushia nini
Na inakuwaje zingine ziwe matenga,na zingine uhesabu mojamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…