Mwenye uzoefu na hizi kazi za kwenye nguzo Dar-es-Salaam

Emmanuel180

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2019
Posts
342
Reaction score
626
Ebhan hapa Dar unaweza pita kwenye nguzo wamebandika tangazo la kazi mara nyingiiiiii mnooo mfano Ds max wanahitaji watu wa kazi wanakuandikia kabisa mshahara may be 275k nafasi za kazi zimegawanyika mfano.
  • Ofisini
  • Store keeper
  • Usambazaji
  • Udereva
N.k

Nataka kujua kwa wenye uzoefu wa hizi kaz unakuta mfano fomu unalipia 2000 je ni kwel hizi kazi hua zinakuepo na mshahara hauna longo longo na je kazi hizo za usambazaji udereva hua ni bodhaa gani inasambazwa kwa wenye uzoefu nahizi kazi na je probability ya kupata hizi kazi ikoje kama ni nzuri hazina shida.
 
Unakuta ukiwa dar kuna kampuni nyingi zinabandika matangazo kila mahala kwenye nguzo wanaandika na mshahara mfano 275k sasa apaa mi hua nawaza hizi kamupuni zinafanya biashara gani maana ukienda hawakwambiii mpk siku ya kujaza mkataba.

Tatizo niki andika uzi kama huu moderators wanafuta niliandika hata dk 5 hazijapita sijauona sijui kwann mnafanya hv na sahv ni mara ya 3 naandika wanaufuta.

Naomben kujua changamoto za hizi kaz mfano unakuta kampuni inajiita ds max na zinginezo hapa dar unakuta wana nafasi zao kama storekeeper usafirishaji na na mambo kama ofisini n.k

Je, wenye uzoefu na hizi kazi mna lipi la kunishauri.
 
Kazi zinakuepo lakini mara nyingi ukifika huko unakuta ni kazi ya machinga kuuza vyombo utalipwa KULINGANA na mauzo yako kwa siku. Ipo HIVYO tu.
 
Excatly hawa mara nyingi kazi zao huwa ni za kuuza vyombo mfano, chupa za chai , mabeseni, madiaba, nk malipo yake ukiuza chombo labda bei elekezi beseni moja 4000 ww ukiuza 6000 basi kile cha juu ndio malipo yako
 
Mara nyingi hizo zinakuwaga zile za kutembeza vyombo.
Umenikumbusha mbali mana Kuna kipndi mdogo wangu alikuwa anatafuta kazi akaangukia kwa hao jamaa.
Mbaya zaidi wao walipelekwa vijijini ndani ndani huko kwa wamasai aliporudi analalamika miguu inauma mana alitembea sana.
Mbaya zaidi hawajauza chochote.
Haya maisha ukiwa unatafuta kazi unakutana na kila adha.
 
Unapokubali Ajira maana yake umeridhika na utazingatia makubaliano(Mkataba). Je mdogo wako aliusoma vizuri na kuuelewa huo Mkataba kabla ya kutia saini yake? Au yy aliangalia tu kwamba hapa naajiriwa mengine tutajuaga huko mbele.
Angalizo: Biashara iwe yako au ya kuajiriwa i.e unamfanyia Tajiri mwenye hiyo biashara ni lazima suala la soko liwe ni bayana. Je, ww mwajiriwa ndiye utakayetafuta soko la bidhaa hiyo (e.g. mmachinga anatafuta soko) au soko atakutafutia Tajiri? (e.g.ataweka kibanda(Duka) na ww Mwajiriwa unamsubiri mteja ambaye huna ahadi naye) kwa hiyo ninachotaka kusema hapa ni Mdogo wako kulalamika eti alipelekwa masaini na alitembea sana. Hakujua Nature ya kazi aliyokubali kuajiriwa? Kumbe makampuni hayo yapo-yapo tu halafu Vijana wanaingia huko bila kujua yaliyomo halafu wanalalamika.
Lakini nakushukuru Feitty kwani hata huku Umasaini kwetu tunayaona matangazo ya namna hiyo kwenye nguzo za umeme - kumbe ndo mambo hayo. Nimejifunza kitu.
 
Kazi zinakuepo lakini mara nyingi ukifika huko unakuta ni kazi ya machinga kuuza vyombo utalipwa KULINGANA na mauzo yako kwa siku. Ipo HIVYO tu.
Sio matapeli ila TANGAZO Lina mvuto lakini nyuma ya pazia bora muokota makopo
 
Unapokubali Ajira maana yake umeridhika na utazingatia makubaliano(Mkataba). Je mdogo wako aliusoma vizuri na kuuelewa huo Mkataba kabla ya kutia saini yake? Au yy aliangalia tu kwamba hapa naajiriwa mengine tutajuaga huko mbele.
Angalizo: Biashara iwe yako au ya kuajiriwa i.e unamfanyia Tajiri mwenye hiyo biashara ni lazima suala la soko liwe ni bayana. Je, ww mwajiriwa ndiye utakayetafuta soko la bidhaa hiyo (e.g. mmachinga anatafuta soko) au soko atakutafutia Tajiri? (e.g.ataweka kibanda(Duka) na ww Mwajiriwa unamsubiri mteja ambaye huna ahadi naye) kwa hiyo ninachotaka kusema hapa ni Mdogo wako kulalamika eti alipelekwa masaini na alitembea sana. Hakujua Nature ya kazi aliyokubali kuajiriwa? Kumbe makampuni hayo yapo-yapo tu halafu Vijana wanaingia huko bila kujua yaliyomo halafu wanalalamika.
Lakini nakushukuru Feitty kwani hata huku Umasaini kwetu tunayaona matangazo ya namna hiyo kwenye nguzo za umeme - kumbe ndo mambo hayo. Nimejifunza kitu.
Umeongea point japo hujaweka picha
 
Umeongea point japo hujaweka picha
.
image-muUdekToNRRyMPiO.jpg
 
Enzi hizo niliingia kwenye mtego wa hao jamaa! Nimetoka zangu kijijini huko, nikawapigia simu bhana ili kujua namna ya kufika ofisini kwao! Si unajua tena nilkuwa nimechoka maidha ya kitaa, baada tu ya kuhitimu shule! Halafu mshahara elfu 30 - 50 kwa mwezi! 😋 Ilikuwa ni pesa nyingi sana kwa kipindi hicho. Wakanipa ramani mpaka nikafika Magomeni Mikumi!

Nafika ofisini siku hiyo hiyo nikaondoka na mkufunzi aliye bobea kwenye hiyo shughuli ya promotion kwa ajili ya mafunzo ya siku moja! Tukaizunguka karibia Dar yote kwa miguu! Fah! Na like jua! Kutoka Magomeni Mikumi mpaka Posta 😩

Tunarudi ofisini saa 10 jioni, naambiwa nimefuzu mafunzo! Hivyo kesho nirudi asubuhi kwa ajili ya kwenda kutembeza bidhaa peke yangu! Wakanipa eti na nauli! 😁 Kama nilirudi hiyo kesho!!!
 
Unapokubali Ajira maana yake umeridhika na utazingatia makubaliano(Mkataba). Je mdogo wako aliusoma vizuri na kuuelewa huo Mkataba kabla ya kutia saini yake? Au yy aliangalia tu kwamba hapa naajiriwa mengine tutajuaga huko mbele.
Angalizo: Biashara iwe yako au ya kuajiriwa i.e unamfanyia Tajiri mwenye hiyo biashara ni lazima suala la soko liwe ni bayana. Je, ww mwajiriwa ndiye utakayetafuta soko la bidhaa hiyo (e.g. mmachinga anatafuta soko) au soko atakutafutia Tajiri? (e.g.ataweka kibanda(Duka) na ww Mwajiriwa unamsubiri mteja ambaye huna ahadi naye) kwa hiyo ninachotaka kusema hapa ni Mdogo wako kulalamika eti alipelekwa masaini na alitembea sana. Hakujua Nature ya kazi aliyokubali kuajiriwa? Kumbe makampuni hayo yapo-yapo tu halafu Vijana wanaingia huko bila kujua yaliyomo halafu wanalalamika.
Lakini nakushukuru Feitty kwani hata huku Umasaini kwetu tunayaona matangazo ya namna hiyo kwenye nguzo za umeme - kumbe ndo mambo hayo. Nimejifunza kitu.
Hawakuambii chochote
Unaambiwa tu njoo siku fulani utakapoenda ndio utakachokutana nacho.
Matangazo yao yamekaa kiushawishi hasa kwa watu waliosomea mambo ya biashara kumbe biashara yenyewe ndio kutembeza vyombo.
 
🙏 🙏
 
d

Dah hata mimi nimewahi kumbana na huu msala, pale palm village kwa Warioba Mikocheni, kumbe ishu yao ilikua kutembeza D.light mjini malipo ni commision aiseeh nilidata,ukicheki nilisafiri kutoka mkoani nauli ya kurudi nikawa sina. nikaamua kujichanganya tukuishi kwa washikaji mpaka pale nilipo pata nauli ya kurudi homu
 
Back
Top Bottom