Mwenye Uzoefu na Kuuza Mikungu ya Ndizi Mbichi

Toka uandikage hakuna aliyechangia,labda hakuna anayefqnya hii biashara
 
Sija wahi kusafirisha ila ninacho kijua (sio kwa undani) una nunua mkungu kijijini una tafuta gari la kusafirisha mpaka sehemu husika mfano Dar soko kuu la ndizi (Mabibo)

Huko kijijini uliko nunua lazima ulipe kodi ya mazao ambayo haiwezi kuzidi TZs 1,000 kwa kila mkungu ili upate kibali cha kusafirisha mzigo wako, pia kuna wapakizi nafikiri huwa wana lipwa Tzs 300 kwa kila mkungu

Gharama za kusafirisha zina kuwa kubwa sana ila ina tegemea na unako toa mzigo ni wapi? Mfano mbeya mkungu mmoja sii chini ya Tzs 7,000 - 10,000 Moshi kilimanjaro ni 6,000 - 9000 kuhusu kagera,bukoba na chocho zote zinako patikana ndizi kama rusumo n.k sina uzoefu na hizo anga.

Ukifika Dar mfano ni umeleta soko kuu la ndizi Mabibo (mahakama ya ndizi) ukisha mzigo sokoni mara nyingi magari ya ndizi viazi n.k huwa yanaingia usiku au jioni kwahiyo gari lenye mzigo wako lita lazimika kupaki sehemu salama mtakapo shauriana na Dereva wako ifikapl saa 9 mpaka saa 10 usiku (alfajiri) gari zenye mizigo muda huo ndio huanza kuingia sokoni kwqqjili ya kushusha mzigo na kuuza.

Hapo kwenye mauzo ya mzigo wanatumika madalali kuuza na hapo ndipo umakini unapo hitajika una kabidhiana mzigo na dalali mnaanza kuuza na wewe ukiwepo au kama una mwamini sana una weza kusepa kupiga misele yako, malipo ya dalali kwa kila mkungu atakao uuza ni Tzs 1,000

Pia kuhusu kulipa nauli ya mzigo sio lazima kulipa cash kwa sababu wafanya biashara huwa wana lipa baada ya kuuza mzigo wao, hapo hapo nakukumbusha kuna kodi utakayo ilipa, hii ni kodi ya mzigo wote ambayo mgungu mmoja ni kama Tzs 300 ila sina uhakika sana kuhus kiasi hiki nime sahau kidogo (sorry) pia kuna malipo ya makuli watakao shusha mzigo wako hawa wanalipwa Tzs 300 kwa mkungu mmoja.

Cha mwisho kabisa kua makini sana na madalali kjna wengine ni matapeli kuna wengine ni wazuri na ni wema sana, hakikisha una kua makini na una fanikisha biashara yako nakutakia kilala kheri mwenyezi mungu akutangulie mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…