Mwenye uzoefu wa kununua gari car trade view, je ni waaminifu

Mwenye uzoefu wa kununua gari car trade view, je ni waaminifu

sambu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
285
Reaction score
283
Nimeisha negotiate bei na cratrade view na nipo stage ya kulipia. Mwenye uzoefu na hawa jamaa anijuze nisije ingia mkenge.
 
Trade car view hawauzi magari wenyewe wana host tu makampuni yanayouza magari na yapo mengi mengine ya kitapeli na mengine ni ya ukweli ungeweka jina la kampuni watu wangekusaidia otherwise make sure unalipa kwa kutumia paytrade ndo utakuwa na uhakika wa kutotapeliwa
 
Trade car view hawauzi magari wenyewe wana host tu makampuni yanayouza magari na yapo mengi mengine ya kitapeli na mengine ni ya ukweli ungeweka jina la kampuni watu wangekusaidia otherwise make sure unalipa kwa kutumia paytrade ndo utakuwa na uhakika wa kutotapeliwa

Agreed...Trade car view ni kama forum ambayo makampuni yanaweka biashara zao za magari. Ukilipia kwa paytrade, maana yake ni kwamba trade car view wataipokea na kuitunza pesa yako mpaka utakapo-confirm kwamba gari umelipokea salama then wana -release the money to the concerned supplier/ company.
Pia kwenye mtandao wa tradecarview waweze kuona list ya makampuni ambayo ni "blacklisted" kwa utapeli ingawa mengine bado yanaonekana yanatangaza biashara zao kwenye tradecarview....
Nakutakia ununuzi mwema, Mungu akusaidie usitapeliwe!
 
Tradecarview kuna kampuni za ukweli na matapeli.

Ninaweza kukusaidia kufanya ordering mpaka gari inafika kwa fee kidogo hapa dar.

Kama unahitaji huduma hiyo ni PM au nipigie 0753742205
 
Mimi nipo dubai huu ni mwaka wa 5..naomba nikupe ideas kidogo...ununizi wa magari online si mbaya lakini kadri siku zinavyokwenda wahuni wamebuni njia ya kutapeli...moja wanawezakukutangazia gari ukalipenda lakini maelezo yake yakawa sio..kuna bwana alinunua gari akijua ni 2005 kama wale wauzaji walivyomwambia lakini lilivyokaguliwa baada ya kufika port dar likaonekana ni 1999 hiyo ni tofauti kubwa sana ktk model na cost ya gari lenyewe..pili unapofanya mawasiliano na hao watu wa japan kuwamwangalifu sana kuna watu mostly nigerians wana uwezo wa ku track mawasiliano yenu ukajiona unaongea na japan kumbe unaongea na nigeria...tatu ata wajapan wenyewe baada ya kujua wapo kwenye chati kuna watu wanakwenda mnadani kununua magari nao wanapandisha bei na kuyatangaza kwenye net sasa mengi ya magari hayo si yenye ubora sana..chakuzingatia wambie wakutumie vin number yaani chasis number hiyo ndiyo bora kuliko picha ya gari maana ile inakupa details zote za gari ata kama gari liliibiwa sehemu wawezajua...kuna websites nyingine ni nzuri sana hawana longolongo lakini ukweli unabaki palepale the best way to buy a vehicle especially the used ones is physical yaani wewe ulikague kiufundi kabla ya kulichukua..online siyo mbaya lakini sikushauri sana...hapa dubai una nakwenda sana kwenye showroom za magari wanabadirisha kila kitu kuanzia km ngapi gari limetembea nk...good luck...cheap is exp...
 
Nashukuruni kwa ushauri. Kwa wale waliotaka jina la kampuni (seller) inaitwa TOMISHO CO. , LTD. Vipi taarifa zake?
 
Kama ulivyoshauriwa, lipia kupitia paytrade ndiyo njia sahihi ya ku secure pesa yako.
Nashukuruni kwa ushauri. Kwa wale waliotaka jina la kampuni (seller) inaitwa TOMISHO CO. , LTD. Vipi taarifa zake?
 
Nimechagua gari kutoka hapo kwao naenda kulipa kesho ila thru paytrade, nitawashirikisha each stage.
 
Binafsi huwa naagiza gari Japan kupitia Real Motor Japan (RMJ)
Anayehusika na kampuni hiyo ni MIHA MATSUOKA na hivi karibuni alikuwa Lusaka Zambia pamoja na Dar es Salaam Tanzania kwani ndipo kampuni yao inawateja wengi sana

RMJ ni registered katika tradecarview, nimeshaagiza zaidi ya mara 3 na hata sasa natumia bidhaa niliyoipata July 2012
 
Nawashukuruni kwa ushauri wenu. Nimebadirisha na kuamua kulipa kupitia paytrade.Nalipia kesho. Nitawapa experience yangu.
 
Kabla ya hapa niliisha agiza gari toka Autorec. Hawa jamaa ni waaminifu ingawa bei za magari yao zipo juu kidogo. Nililipa kwa njia ya TT na kila kitu kilienda sawa. Hivyo mtu akipata gari huko, anaweza kuagiza bila shida.
 
Hili ndio jamvi bwana, Kweli hii ni Information Era,
Kila kitu wazi ukipigwa umejitakia mwenyewe.......! Na hili jukwaa la biashara wanafika watu wachache sana wakati dhahabu ndio iko huku.
 
Hili ndio jamvi bwana, Kweli hii ni Information Era,
Kila kitu wazi ukipigwa umejitakia mwenyewe.......! Na hili jukwaa la biashara wanafika watu wachache sana wakati dhahabu ndio iko huku.

Hakika mkuu Mwanahisa upo 100% right
 
Sambu, itakuwa vema umelipia kwa paytrade, itakuondolea presha mali utaipata bila shaka. Kwa ujumla tu ni kwamba utapeli unaotembea kupitia Cartrade view ni wa kuletewa kitu tofauti na matarajio! Wauzaji wabaya wanachofanya ni udanganyifu tu kuletewa kitu usichotarajia tofauti na kilivyoonekana kwenye mtandao. Inashauriwa kwanza soma history ya muuzaji kaanza lini biashara hiyo, wale wenye siku nyingi kama miaka 7 waaminika namitaji yao mikubwa. Pia angalia maoni ya wateja walionunua kwake! Ila pia usisahau kuwa haya magari ni mitumba siyo mapya kwa hiyo hakuna hata muuzaji mmoja ambaye watu hawajamlalamikia kwamba wametapeliwa! Ukinunua gari used kwenye mtandao na hasa yale ya bei za kutupa likaja kama lilivyoonyeshwa na ukakuta liko safi shukuru sana! Kuna wauzaji kama Autorec hao ni guranteed kupata gari safi maana wao wanaworkshop ambako huyakarabati magari kabla hawajayauza, ila bei zao ndiyo kali kabisa! Car trade view iko juu ingawa kuna matapeli yaani wadanganyifu lakini mzigo wanakuletea wengine kwa mbinde sana kama hukutumia paytrade.
 
Cartrase view (Pay trade) waliisha confirm kupokea pesa na wanawaliana na sypplier. Natarijia kupata soft copy ya documents wiki hii. Jana supplier kanipigia simu kuthibitisha kuwa watajitahidi kutoa huduma nzuri na kuahidi ushirikiano hadi nitakapo pata mzigo. Fingure closed, ila kuna dalili za kufanikiwa. Nimecheck review ya supplier na kuona commets za watu ni nzuri na zipo za watanzania walia agiza magari hata Januari mwaka huu. Kwa wale wenye interest nitawa update ili iwasaidie kwa baadae. Nikiliwa nitawajulisha.
 
Back
Top Bottom