Sambu, itakuwa vema umelipia kwa paytrade, itakuondolea presha mali utaipata bila shaka. Kwa ujumla tu ni kwamba utapeli unaotembea kupitia Cartrade view ni wa kuletewa kitu tofauti na matarajio! Wauzaji wabaya wanachofanya ni udanganyifu tu kuletewa kitu usichotarajia tofauti na kilivyoonekana kwenye mtandao. Inashauriwa kwanza soma history ya muuzaji kaanza lini biashara hiyo, wale wenye siku nyingi kama miaka 7 waaminika namitaji yao mikubwa. Pia angalia maoni ya wateja walionunua kwake! Ila pia usisahau kuwa haya magari ni mitumba siyo mapya kwa hiyo hakuna hata muuzaji mmoja ambaye watu hawajamlalamikia kwamba wametapeliwa! Ukinunua gari used kwenye mtandao na hasa yale ya bei za kutupa likaja kama lilivyoonyeshwa na ukakuta liko safi shukuru sana! Kuna wauzaji kama Autorec hao ni guranteed kupata gari safi maana wao wanaworkshop ambako huyakarabati magari kabla hawajayauza, ila bei zao ndiyo kali kabisa! Car trade view iko juu ingawa kuna matapeli yaani wadanganyifu lakini mzigo wanakuletea wengine kwa mbinde sana kama hukutumia paytrade.