Mwenyekiti aliondoa watu kwa mbinde Kimara Stop Over, jioni ajali mbaya ikatokea

Joined
Oct 6, 2024
Posts
147
Reaction score
303
Lori lililoparamia Watu usiku wa kuamkia leo February 14,2025 Kimara Stop Over Jijini Dar es salaaam na kusababisha vifo vya Watu watatu, limeondolewa eneo la tukio huku Madereva bodaboda wa eneo hilo wakisema jana asubuhi kabla ya ajali, Mwenyekiti wa Mtaa alijitokeza na kuwaomba Watu wasikae kwenye eneo hilo kwakuwa lipo karibu na barabara na kwamba kama sio agizo la Mwenyekiti huenda majanga yangekuwa makubwa zaidi.

#AyoTV imefika eneo la tukio na kuona Watu wakiendelea na shughuli zao kama kawaida ambapo Dereva bodaboda mmoja amenukuliwa akisema “Jana asubuhi ilikuwa kama bahati tu akaja Mwenyekiti akawa anawasogeza wasogee maeneo sahihi ndio maana vibanda vimesogezwa pembeni imekuwa kama bahati tu”

“Sababu zake ilikuwa hizohizo (kuwaepusha na ajali) ni kama kawaokoa mwanzoni walibishiabishia lakini Mwenyekiti alijitahidi wakatii sheria, kabla ya hapo vibanda vilikuwa vingi, Mwenyekiti tunamshukuru sana kuwasogeza sijui idadi ingekuwaje” #MillardAyoUPDATES

 
Hayo yanaitwa maono
 
Anaangushaje gari eneo lisilo na kona wala mteremko mkali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…