Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Deogratius Mahinyila anazungumza na Vyombo vya Habari muda huu akizungumzia sakata la utekaji nchini huku akianza kueleza namna ambavyo Amani Manengelo, Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, alivyotekwa na kupotea tangu tarehe 14.02.2025 huko Misungwi
Alichozungumza Deogratius Mahinyila
"Amani Manengelo ni mkazi wa Old Misungwi, ana rafiki yake wa kike (aliyepewa jina la P) yeye anafanya kazi ya ususi alipokea simu kutoka kwa mdada ambaye hamfahau alimpigia simu akimwambia anahitaji huduma ya kusuka. Baada ya muda mteja aliyempigia simu huyo P alifika eneo lile wakiwa wawili walipofika walimkuta P akiendelea kumsuka mtu mwingine."
"Mteja alipofika akamwambia P mimi sihitaji kusukwa tunamtafuta Amani Manengelo. Walikuwa wanajua P na amani Manengelo wana mawasiliano. Hivyo wakamwambia tunamtaka kwa sabau alitumiwa pesa kiasi cha milioni tano kimakosa hivyo wanamtaka ili atoe hizo pesa. Wakaongezeka wanaume wawili wakamfunga P na pingu wakamuonyesha bunduki wakamtisha kuwa afuate maelekezo na asipofuata watamfanya kitendo kibaya."
"Wakampa maelekezo ampigie simu Manengelo akamwambia kuna dharura nyumbani kwake. Kwa sababu Amani alikua kazini akamwmbia nimebanwa na majukumu nitakuja baadae. Ipofika majira ya saa mbili usiku Amani akarudi nyumbani na anaishi na rafiki yake pale nyumbani. Baada ya kurudi Amani akamwambia rafiki yake naenda kwa P aliniambia ana shida. Baada ya Amani kwenda kwa P hapo ndio ukawa mwisho wa kuwa kwake uraiani"
"Mara zote Mkuu wa Mkoa (wa Mwanza Saidi Mtanda) amekua akisema hadaharani kwamba jambo hili linafanyiwa kazi na Amani Manengelo atapatikana, kwahiyo mpaka sasa hatua ambazo zimekuwa zikisemwa na Mkuu wa Mkua wa Mwanza na Serikali ni kwamba ahadi tulinayo kama Bavicha na Chama (CHADEMA) pamoja na ndugu zake Amani Mandengelo ni kwamba Amani Manengelo atapatikana"
"Leo tarehe 4 Machi, 2025 zimetimia siku 18 toka siku aliyotekwa na kupotea Katibu wetu Amani Manengelo huku Misungwi Mkoa wa Mwanza. Ni maoni yetu kwamba kwa namna tulivyofuatia suala hili ndani ya siku hizi 18 na kuzingatia kauli na vikao ambavyo viongozi wetu wa Bavicha na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Victoria pamoja na Jeshi la polisi Mwanza sisi binafsi kuna maswali tunajiuliza na maswali haya tuna waalika Watanzania na wenyewe wajiulize maswali haya, lakini pia tunatamani maswali haya Jeshi la polisi na Serikali watujibu kwasababu tusipopata majibu ya maswali haya yako mambo ambayo sisi tunaamini yatakuwa ni kweli"
"Asilimia kubwa ya vijana ambao wanatekwa ni vijana wa upinzani ni vijana WanaCHADEMA ni vijana wanaharakati. Kwa kuwa watu wanaotekwa ni watu wenye mrengo huu wa kimageuzi ni watu wanaoiunga CHADEMA hebu tuambieni kwa nini tusiamini kutekwa kwao mnataka kupunguza ari na morali ya vijana wa upinzani kuendelea kuikosoa serikali kwa nini tusiamini huu ni mkakati wa kupunguza kasi yetu ya kuwa wapinzani."
"Ni kikundi gani kina maslahi na vijana wa CHADEMA. Polisi mtuambie hawa watu ambao wanaotuteka vijana wa chadema wanaowateka vijana ambao wana maoni tofauti na serikali"
Soma, Pia