Mwenyekiti Bunge la Katiba wapambe wa Chenge waelekeza nguvu kwa Migiro,Chikawe

Mwenyekiti Bunge la Katiba wapambe wa Chenge waelekeza nguvu kwa Migiro,Chikawe

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
sitta1.jpgSitta download.jpg Migiro download (1).jpg Chikawe

  • Chenge baada ya kutouzika huenda akaweka jezi bagani
  • Wapambe wake waelekeza macho kwa Migiro na Chikawe
  • Sitta aendelea kuwa mwiba kwa kundi hilo

Kampeni za makundi ya vigogo wanaopigana vikumbo kugombea uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba zimechukua sura mpya, baada ya kundi lililokuwa likimuunga mkono Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge kudaiwa kubadili ghafla mwelekeo wa kampeni zake.

Habari za kuaminika zilizopatikana mjini hapa jana zilieleza kuwa kundi hilo lililokuwa likimtaka Chenge, sasa linataka nafasi hiyo iwaniwe na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro au Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

Hatua hiyo inadaiwa kuchukuliwa na kundi hilo baada ya kubaini kuongezeka kila uchao kwa nguvu za Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye tayari ameshatangaza kuwania nafasi hiyo, huku zile walizozitarajia kutoka kwa Chenge zikizidi kushuka.

Habari hizo zinaeleza kuwa uthibitisho wa hilo, ni ujasiri ulioonyeshwa na Sitta aliyeamua kutangaza hadharani azma yake ya kuwania nafasi hiyo, huku Chenge akishindwa kuthibitisha kuwa atagombea ama la.

Uchaguzi wa mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba unatarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii baada ya Bunge hilo kupitisha azimio la kuipitisha rasimu ya kanuni za Bunge Maalumu kesho.

Awali, Chenge aliiambia NIPASHE kuwa hayuko tayari kutangaza kama atagombea nafasi hiyo au la kwa kuwa kanuni za Bunge hilo bado hazijatungwa.

Kauli kama hiyo iliwahi pia kutolewa na Waziri Sitta katika siku hiyo hiyo, ambayo Chenge aliashiria kusubiri kanuni.

Hata hivyo, siku chache baadaye, hata kabla ya rasimu ya kanuni hizo haijapitishwa na Bunge, Waziri Sitta alitangaza azma yake ya kugombea nafasi hiyo kwa maelezo kwamba, anataka kutimiza ndoto ya Rais Jakaya Kikwete ya kupata katiba bora.

Jumatatu wiki hii, Chenge alipoulizwa na NIPASHE kuhusiana kinyang'anyiro hicho, alikataa kuzungumza na badala yake akamtaka mwandishi aendelee na shughuli zake.

Waziri Chikawe alipotafutwa na NIPASHE jana kuzungumza kama ana nia ya kugombea nafasi hiyo au la, alimtaka mwandishi kuvuta subira kwa kuwa wakati huo hakuwa na nafasi ya kuzungumza.

Dk. Migiro ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Jitihada za kuwatafuta viongozi hao wanaotajwa kuwania nafasi hiyo zinaendelea.



CHANZO: NIPASHE

 

Attachments

  • sitta.jpg
    sitta.jpg
    42.6 KB · Views: 152
Nguvu za Chenge ni kwa Chikawe, Migiro ni kundi moja na Sitta ......Membe ....hivyo Chikawe ndio kundi la Lowassa na Chenge ...
 
Uchunguzi uliofanyika na Gazeti nipashe dalili za wazi Chenge kuvua jezi na kuiweka begani ni kubwa ndio sababu ya wapambe wake kuanza kuangalia mbadala wakiangaza huku na kule wanajaribu kutupa karata kwa Migiro na Chikawe kuimarisha nguvu zao huko kushindanda na Sitta.
 
Chikawe ni zao la Lowassa , unakumbuka wakati wa sakata la Chenji ya rada alitoa kauli gani? Migiro ni mteule wa watawala
 
Chikawe ni zao la Lowassa , unakumbuka wakati wa sakata la Chenji ya rada alitoa kauli gani? Migiro ni mteule wa watawala

Naona kuna logic hapa, Sitta alishafanyiwa mizengwe tangu uspeaker wa bunge la Jamhuri sidhani akawa mteule wa watawala, kwa bafasi ya sasa chama hakina ubavu kuingilia uteuzi wa wajumbe, kinachofanyika ni kuingiza watu wao ili kujaribu kudhoofisha nguvu za Sitta.
 
Back
Top Bottom