Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Juma Kassim Ndaruke ametoa rai kwa wa Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi Kibiti kusimama kidete na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutafuta kura za Urais kwenye kila eneo la Wilaya Kibiti.
Ndaruke ametoa rai hiyo katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliofanyika Kibiti Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki ambapo amesisitiza Wanawake kutafuta kura za kutosha Kwa Rais Samia.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema Wanawake wana deni kubwa 2025 kwa kuhakikisha wanafanya jitihada za kutosha za kutafuta kura za urais kwenye kila pembe ya mtaa ya wilaya kibiti kwani mgombea wa Urais ametoka kwenye umoja wa wanawake ССМ.
"Tusije kucheza na mtu yoyote mwenye virishia vya kutaka kupungua kura za chama cha mapinduzi kwenye maeneo yote, niwaombe sana tusije kuthubutu kucheza na kudharau mipango yoyote itakayoleta viashiria vya kupunguza kura za Dkt Samia kwenye maeneo tunayongoza, tukiruhusu mipango sisi ndo tutakuws tumeyahudumu, twende kwa nguvu kubwa kuhakikisha wilaya ya kibiti inakwenda wilaya kwanza kutafuta kura za mgombea wa urais 2025." amesema Ndaruke
Ameongeza kuwa katika kipindi cha uchaguzi wapo wamama wamepanga kugombea na wengine kutetea nafasi zao isije ikawa vita kwa wanaotetea nafasi zao, wale waliojiandaa kugombea na kutete nafasi zao wakatetea kwa nguvu zote.
Aidha Ndaruke amesema nafasi hizo ni mali ya chama cha mapinduzi haina haja ya wanachama kugombana kwenye kugombea nafasi hizo huku asisitiza kuheshimu kanuni na taratibu za chama cha mapinduzi.