Mwenyekiti CCM Singida (M) Martha Mlata: Miaka 60 ya Mkoa wa Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MWENYEKITI CCM (M) MARTHA MLATA KATIKA ZIARA YA RAIS SAMIA MKOA WA SINGIDA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ndugu Martha Mlata ameambatana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ziara ya kukagua miradi na kuzindua miradi mbalimbali ndani ya Mkoa wa Singida

Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Singida imeambatana na kuadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwa Mkoa wa Singida uliozaliwa tarehe 16 Oktoba, 2023 tangu kuanzishwa kwake.

Rais Samia Suluhu Hassan amekagua na kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo mkoani Singida ikiwemo Ufunguzi wa Shule ya Msingi Imbele, mabweni ya madarasa ya Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein; Kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya kiwango cha Lami kutoka Makongorosi-Rungwa-Noranga-Mkiwa sehemu ya Mkiwa-Itigi-Noranga km 56.9; Ufunguzi wa Jengo la Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ikungi; Ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama.

Viongozi mbalimbali wamekula Keki kusherehekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Singida katika Uwanja wa Bombadia mkoani Singida leo tarehe 16 Oktoba, 2023 ambapo Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
 

Attachments

  • F8eiZJ9WAAAGZnn.jpg
    94.2 KB · Views: 5
  • F8hRStyXQAEI_w3.jpg
    80.4 KB · Views: 4
  • F8fCM0BXwAAUixX.jpg
    96.3 KB · Views: 4
  • F8kQ0dwWwAAY5XI.jpg
    265.2 KB · Views: 4
  • F8kQ0d1W0AADYcT.jpg
    235.3 KB · Views: 5
  • F8kSry0XkAASN6l.jpg
    97.2 KB · Views: 1
  • F8kDEESWYAA__FQ.jpg
    60.6 KB · Views: 3
  • F8jgc2nW8AAaEDQ.jpg
    85 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…