Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Tanga na Mbunge wa Korogwe Vijijini watoa michango ya Milioni 7 kila mmoja ili kununua madawati 200

Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Tanga na Mbunge wa Korogwe Vijijini watoa michango ya Milioni 7 kila mmoja ili kununua madawati 200

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Misaada na michango imeendelea kububujika kutoka kwa viongozi wa CCM

Hii michango kwanini hatukuiona miaka mitatu nyuma?

=================================

Katika kusherehekea miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu, Rajabu Abdulrahaman, ametembelea katika Shule ya Sekondari Mgwashi iliyopo Korogwe Vijijini Kata ya Mngwashi na kutoa mchango wa shilingi milioni saba (7,000,000) kwa ajili ya kununua madawati 100.

Naye Mbunge wa jimbo hilo, Timotheo Mzava, alichangia shilingi milioni saba (7,000,000) ili kukamilisha ununuzi wa madawati mengine 100.

Mwenyekiti Abdulrahaman alisisitiza kuwa CCM inatekeleza kwa vitendo kutatua changamoto za wananchi, huku akiwataka viongozi wa vyama vingine kuacha malalamiko na badala yake wachukue hatua stahiki.

Kuhusu kero ya ucheleweshaji wa ujenzi wa zahanati, Mwenyekiti Rajabu ametoa maagizo kwa uongozi wa halmashauri kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 1 Aprili 2025, zahanati hiyo iwe imeanza kutoa huduma kwa wananchi.

 
Back
Top Bottom