Chama cha Demokrsia na Maendeleo CHADEMA Jimbo la Geita Mjini kimesema hakiko tayari kuwaona baadhi ya Watendaji wa Kata na Mitaa wanashindwa kufuata sheria na taratibu za uchaguzi hasa katika Maeneo ambayo Viongozi wao wanatuhumiwa kuenguliwa kugombea kabla ya kurudishwa.
Hayo yameelezwa Mjini Geita na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Geita Mjini Bi. Pasquina Lucas wakati akinadi Viongozi mbalimbali wanaongombea nafasi za Uenyekiti katika Jimbo la Geita Mjini huku akisema atakaeshindwa kutekeleza wajibu wake sheria itafuata mkondo wake.