LGE2024 Mwenyekiti CHADEMA Katavi: Mkishapiga kura nendeni kwa Mtendaji mwambieni ukipindua matokeo sisi tunapinduka na wewe!

LGE2024 Mwenyekiti CHADEMA Katavi: Mkishapiga kura nendeni kwa Mtendaji mwambieni ukipindua matokeo sisi tunapinduka na wewe!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,


Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela, ametoa wito kwa wakazi wa mtaa wa Kachoma, kata ya Makanyagio, jimbo la Mpanda Mjini, kuwanyima kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika Novemba 22, 2024, Kunchela amekosoa vikali utendaji wa CCM, akidai kuwa wamekuwa wakikosa uwajibikaji na kuwabagua wananchi kwa misingi ya vyama.

Kunchela ametoa mfano wa changamoto za soko hilo, akisema kuwa wananchi wanaendelea kufanya kazi katika mazingira magumu bila huduma muhimu kama vyoo, huku CCM ikijenga miundombinu kwa lengo la kushawishi wapiga kura:

"Kama utapokea pesa ili kuwapa CCM kura, na unafanya kazi kwenye mazingira magumu ya biashara kama haya kwenye soko hili, halafu hakuna hata choo, yaani mnakuja kujengewa sasa hivi kwa sababu tunakwenda kwenye uchaguzi... niwaombe mfanye maamuzi sasa kwa kuwanyima kura CCM."

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Kunchela pia amelalamikia ubaguzi unaofanywa na viongozi wa CCM katika ugawaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri inayotolewa kwa vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu. Amesema kuwa mikopo hiyo mara nyingi hugawiwa kwa kuzingatia itikadi za kisiasa badala ya mahitaji ya wananchi:

"Wenzenu wanagawa mikopo kwa kuangalia jina la mtu fulani, huyu ni Mwanaccm, huyu tunamfahamu hapa mjini. Halafu nyinyi watoto wa mjini mpo hapa mnabaguliwa."

Kunchela amewataka wakazi wa kata ya Makanyagio kuwachagua wagombea wa CHADEMA, akisema kuwa wagombea hao watahakikisha miradi yote inayokuja kwenye kata na mitaa yao inawanufaisha wananchi wote bila ubaguzi. Pia amesisitiza kuwa viongozi wa CHADEMA watakuwa wenye huruma na uwajibikaji:

"Wagombea hawa wa CHADEMA ninaamini watashirikisha miradi yote inayokuja kwenye kata hii pamoja na mitaa yao, watawajibika, watakuwa na huruma. Msichague viongozi wakatili."
 
Inatakiwa wanaopindua matokea ni kuwachoma moto tu ikitokea wakichomwa moto kama watendaji mia tano hivi huu ujinga utabaki kuwa historia hakuna anayetaka kugeuzwa ndafu.
 
Back
Top Bottom