Pre GE2025 Mwenyekiti CHADEMA Kibiti atangaza kumuunga mkono Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
1736316541582.png

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani Mohammedi Seif amejitokeza hadharani na kueleza msimamo wake kuwa anamuunga mkono Freeman Mbowe katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Mwenyekiti wa chama hicho Taifa kwenye mchakato wa uchaguzi wa ndani unaoendelea

Kupitia chapisho lake alilosambaza kwenye mitandao ya kijamii Mohammedi Seif amesema kabla ya kutangaza msimamo wake amekuwa kwenye tafakuri pana, sambamba na kushiriki vikao mbalimbali vya Mbowe anayetetea kiti hicho na mshindani wake wa karibu Tundu Lissu (ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara) ambapo kupitia vikao, na mikutano ya wagombea hao amepata nafasi ya kusikia na kuchuja sera, hoja, maono na mipango ya pande zote

Pia, Soma: Mbowe arudisha fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA

Kupitia chapisho hilo, Mwenyekiti huyo wa CHADEMA wilaya ya Kibiti amesema pia amepata nafasi ya kupitia mahojiano mbalimbali, na kufanya tathmini ambapo kwake aliibua maswali kadhaa kuhusu wagombea hao

"Kwa kipindi chote hiki nilikuwa sijaonesha msimamo wangu juu ya nani namuunga mkono, wakati wa kutafakari nimefanikiwa kushiriki kwenye mikutano na vikao vya Mheshimiwa Mbowe halikadhalika nimeshiriki kwenye vikao, mikutano na mapokezi ya Mheshimiwa Tundu Lissu bila vikwazo vyovyote, pia nimefikiwa kushiriki vikao na wanaomuunga mkono Mheshimiwa Mbowe, vilevile kwa upande wa Mheshimiwa Tundu Lissu, kusudi langu ni kuweza kupata hoja na sera au maono ya pande zote mbili" -Seif

"Pia kupitia mahojiano mbalimbali nilipata nafasi ya kufanya tathmini na kuwa na maswali kadhaa kama;
(i) Nini makusudio ya kila mgombea?,
(ii) Ukweli wa kashfa zinazosukumwa kwa wagombea hao hasa za kuhusishwa ama kutumwa au kutumika na CCM (Chama cha Mapinduzi) ili kukipotezea nguvu chama chetu ili kisiweze kutimiza malengo, na
(iii) Kuvunjwa kwa Katiba hasa katika hoja ya ung'ang'anizi wa madaraka" -Seif

Seif amesema baada ya kufanya tathmini hiyo amepata majawabu mawili makubwa ya kutolewa ufafanuzi, kama vile:-

(a) Tundu Lissu hakuingia kwa nia ya dhati kukikomboa chama hicho bali amesukumwa na watu wenye nia ovu, aidha anatumika kukichafua chama hicho ili kipoteze imani kwa umma na kupoteza uungwaji mkono na kwamba hakujiandaa kugombea nafasi hiyo,

(b) Freeman Mbowe pamoja na kukabiliwa na kadhia za mara kwa mara kama vile kupewa kesi ya ugaidi, kuanzisha harakati ngumu kama maridhiano, kuandaa maandamano nk, kwa lengo la kupambana na watawala (yaani CCM na serikali yake), kuendesha mikutano ya hadhara kwa lengo la kuwafikia wananchi kwa njia za anga na nchi kavu, kuendesha mijadala na majadiliano na taasisi mbalimbali za kijamiii, kuanzisha na kufanikisha ununuzi wa jengo kubwa la ghorofa la chama (makao makuu ya CHADEMA yaliyoko Mikocheni Dar es Salaam), kuimarisha mtandao wa chama hicho, kufanikisha uchaguzi wa ndani ya chama kuanzia ngazi ya matawi, kata, majimbo/wilaya, mikoa na hatimaye Kanda, sasa amejiridhisha pasipo shaka kuwa Mbowe anastahili kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kipindi kingine cha miaka mitano (5) ijayo

"Hivyo basi, natangaza rasmi leo tarehe 07/01/2025 kuwa mimi namuunga mkono Mheshimiwa Mbowe, na pia nawaomba wajumbe wote wa mkutano mkuu wa CHADEMA utakaofanyika tarehe 21/01/2025 kumpa kura zote Mheshimiwa Freeman Mbowe" -Seif
 
View attachment 3195531

Mghegerwa style!
Usiwaamini watu wa Kibiti mana waliwaficha magaidi kwa miaka mingi mpaka wakataka kuvuruga nchi . Kibiti ni mama wa ugaidi Tanganyika .

Hivyo ni lazima wamuunge mkono gaidi Mbowe.
Ni kawaida kwa watu wa Kibiti kuwaficha magaidi na kuwaunga mkono
 
Ndiyo Demokrasia hiyo,CCM wajifunze Kwa Chadema namna Demokrasia inavyoendeshwa, inashangaza chama chenye umri wa mzee hata ustaarabu hawajui
 
Back
Top Bottom