Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara Chacha Heche amemuomba Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira kuacha kutumia majukwaa kutoa kauli tata ambazo hutolewa na vijana kwani akiendelea kufanya hivyo itampunguzia heshima kutokana na umri alionao.
"Mzee Wasira sintomjibu, wazee ni hazina ya hekima na busara asifanye kazi ya UVCCM, aachane na mambo ya vijana afanye mambo kwa umri wake pia, ingelikuwa ni imani yangu Wasira akija Mkoa wa Mara tuweze kwenda kuvuna mambo ambayo sisi hatuyajui kwa sababu ya umri wake sasa naenda kuvuna nini" amesema Heche.