TrioNeTwork
JF-Expert Member
- Aug 7, 2022
- 444
- 382
Kuna mambo tunaweza kubishana pengine ili kulinda itikadi au falsafa zetu ila kamwe hatuwezi kubishana ili kulinda uhalifu na uovu mkubwa kwa kiwango hiki kwenye taasisi kubwa kama CHADEMA.
Nimemsikiliza Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu anasema endapo atashinda na kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa basi atafutilia mbali utaratibu wa mtu mmoja kupita peke yake kwa wadau ili kukusanya fedha kwaajili ya kuendesha na kuendeshea shughuli mbalimbali za chama utaratibu ambao umedumu kwa kipindi Cha zaidi ya Miaka 20 sasa.
Kwa lugha nyepesi huenda ama ni kweli Freeman Mbowe ni mnufaika mkubwa wa fedha za CHADEMA kuliko hata CHADEMA yenyewe kwa miaka hii 20 aliyokaa madarakani,
Najaribu kuwaza ni kiasi gani Cha fedha Mwenyekiti Freeman Mbowe amejizolea toka kwa wapenzi, Wafuasi, wanachama na Viongozi wa CHADEMA wasiotaka kujulikana kwa majina ila tu kwa Mwenyekiti wa Chama Freeman Mbowe kwa kipindi chote hiki Cha miaka 20.
Najiuliza zaidi ni jambo gani lililomfanya Mwenyekiti Freeman Mbowe asitumie kabisa akaunti ya CHADEMA kwa sharti la wadau hao wa CHADEMA kutoandika majina yao rasmi ( watumie fictious names ) kwa lengo la kukuza usiri na kuepa mkono wa CCM na dola.
Mwanafalsafa mmoja wa Kigiriki aliwahi kusema " Yeyote unayemwona mbele yako jua kuwa mtu huyo ni mwizi kwa asili" baada ya falsafa hii ya kila binadamu ni mwizi kwa asili ndio maana utaona leo kila sehemu ya pesa lazima ihusishe watu zaidi ya wawili au wawili mfano hata Password ni mtu wa pili,
Kwa dhana hii ya kila mtu ni mwizi kwa asili, Je falsafa hii haitamuhusu Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa kipindi hiki chote cha zaidi ya miaka 20? Ninani anajua Mwenyekiti huyu kakusanya kiasi gani Cha fedha za wadau hata sasa? Je, hao wadau wataendelea kumwamini Mwenyekiti Freeman Mbowe hata baada ya Uchaguzi huu?
Nahitimisha hivi, kama kweli Mwenyekiti Freeman Mbowe amekuwa akifanya haya kwa miaka yote 20 ya uongozi wake basi Freeman Mbowe ndio Mtanzania pekee aliyejikusanyia pesa nyingi zaidi za Watanzania kwa mgongo wa kuzipeleka CHADEMA na huenda Sasa Uenyekiti wake ukawa wa faida zaidi hata ya Urais wa nchi na madhara yake huenda ikawa ni ngumu zaidi kumwondoa kwenye nafasi hii hasa baada ya kujitengezea Wafuasi binafsi na Vibaraka kwa kutumia michango hiyo ya siri ya Wafuasi, wapenzi na Wanachama wa CHADEMA ambayo haitozwi Kodi, haikaguliwi na CAG wala haijulikani kwa mtu yeyote ila yeye.
Na kwa ujumla wake nimepata na tumepata majiibu ya kwanini Mwenyekiti Freeman Mbowe pamoja na mateso na manyanyaso mengi toka kwa dola na Serikali lakini bado Mwenyekiti huyu anaifurahia nafasi yake hiyo kwa miaka zaidi ya 20.