Mwenyekiti Kitayosce matatani tuhuma za rushwa

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
UONGOZI wa Klabu ya Fountain Gate FC, imemripoti kwenye Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mwenyekiti wa timu ya Kitayosce FC, YUSUPH KITUMBO, kwa tuhuma za kuwarubuni wachezaji wao ili kucheza chini ya kiwango katika mchezo wa Ligi ya championship iliyozikutanisha timu hizo Jana Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Shabiby mjini Gairo ambao ulimalizika kwa timu hizo bila kufungana.

Kwa mujibu wa WENDO MAKAU ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, amesema Mwenyekiti huyo alituma pesa kiasi cha Tsh. Milioni 2 na zaidi kwa Wachezaji zaidi ya watano wa nafasi mbalimbali ili wagawane kiasi hicho cha fedha.

Wachezaji hao waliripoti suala hilo Kwa uongozi wao ndipo uongozi wa Fountain ukaripoti Takukuru na jana kabla ya mchezo na Mwenyekiti huyo wa Kitayosce FC alihojiwa Takukuru na kuacha baadhi ya simu zake kwa hatua zaidi za kiuchunguzi.

Jumanne ya wiki inayoanza Kesho, uongozi wa Fountain Gate utaripoti suala hilo kwenye shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

Alipotafutwa Kwa nyakati tofauti Mwenyekiti huyo ili kupata kauli yake juu ya suala hilo, simu yake haikupatikana hewani.

Chanzo: Kitenge Sports
 
Watakufa maskini hao wachezaji
 
Yusuph kitumbo,hivi bado ana yale Mabus yake? Alikuwa Lecturer AMUCTA.

Kumbe ndiyo Mwenyekiti wa hiyo timu? Aisee, wangekula hela alafu wakaze uwanjani kama kawaida. Hakukuwa na mkataba. Vitu vingine nchini kwetu bado ni vya hovyo.
 
Kitayosce wameona huu mwaka wa nne wanaishia playoff,wameamua kutumia nguvu
 
Back
Top Bottom