TANZIA Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE

Chief lazima aende na msaidizi ,wajiandae hakuna namna ,mmojawapo,ataungana nae,ni utaratibu,stay tuned
 
RIP Mzee Mengi..

Huu Uzi umepunguaje comments Kuna zinazofutwa? Maana nilikuwa page ya 41 ghafla naenda 45 narudishwa 35!
Kuna comments zinafutwa. Zinatakiwa zibaki za RIP tu.Mbwembwe zingine no.
 
P
Wanataka kuficha nini?Au kila mtu ajadili wanachotaka kusikia wao?Uzi ulikua umetembea sana,leo naona umerud nyuma sana.

Nilisha washtukia siku nyingi, baadhi ya mods wana ajenda zao za siri - wanachangamkia sana comments zinazo inanga Serikali au Chama tawala - lakini ki akiwa muzzled wanakimbilia Mahakamani kutaka watendewe haki - nachukulia modus operandi ya namba hiyo kama hypocrisy iliyopitiliza mipaka, niliwahi kutia maoni yangu kuhusu ubaya wa GMO kutumikaNchini comments zangu zilikuwa pulled down usiku wa manane on whose interest? Na hii haikuwa mara ya kwanza kutendewa hivyo - mtu unabaki unashangaa in case of anything mbona majina yetu alisi yanajulikana kwani tatizo liko wapi? Ndio maana binafsi nimepunguza sana kuchangia.
 
Kuna comments zinafutwa. Zinatakiwa zibaki za RIP tu.Mbwembwe zingine no.
Wewe unatakaje mkuu, si tuko kwenye kipindi cha maombolezo.... Mbwembwe tena za nini??? Eti inasemekana wakiwa Dubai, sijui nini... Ili iweje. Tusubiri mazishi, kama kuna ya kusemwa tutayasikia.
 
Wewe unatakaje mkuu, si tuko kwenye kipindi cha maombolezo.... Mbwembwe tena za nini??? Eti inasemekana wakiwa Dubai, sijui nini... Ili iweje. Tusubiri mazishi, kama kuna ya kusemwa tutayasikia.
Basi sawa.
 
Mkuu, naomba na historia ya mkewe Jacqeuline Ntuabaliwe.
 
"JAMIIFORUMS ~ Where We Dare To Talk Openly" Mbona kauli mbiu hii haiendani na kilichofanyika kwenye uzi huu, comments nyingi zimefutwa kwa manufaa ya nani au watu wa St Peters pale washaingia ofisini kwenu
 
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dr. Reginald Mengi utawasili nchini siku ya Jumatatu- Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo.

Mwili wa Dr. Reginald Mengi utaagwa siku ya Jumanne Mei 7, katika viwanja vya Karimjee- Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo.

Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame, ibada ya mazishi ni siku ya Alhamis wilayani humo kanisa la Kisereni (KKKT)- Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo.
 
RIP MZEE WETU. BINAFSI NILIMKUBALI SANA HUYU MZEE KWA UBUNIFU NA KUPENDA KWAKE WALAU WATU FULANI WAENJOY MAISHA KWA KUFANIKIWA KIMAISHA. PIA MISAADA YAKE KWENYE MASHULE, WALEMAVU, WAHITAJI ULITIA FORA. ILA SIKUBAHATIKA KUKUTANA NAYE.
 
najuliza sana sana kwa nini TBC waliweka maandishi yanayosomeka THE BILLIONARES CLUB wakati wanatujuza kuhsu kifo cha Dr.Mengi??!!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…