- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu Salaam nimekutana na taarifa mtandaoni ikisema kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, pamoja na wanachama wao zaidi ya 60, wamehamia Chama Cha Mapinduzi CCM, Uhalisia wa taarifa hii umekaaje?
- Tunachokijua
- Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Oktoba 8, 2024, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoa wa Simiyu, amefanya ziara ya kikazi katika eneo la Luguru wilaya ya Itilima mkoani humo.
Kutokana na mkutano huo kumekuwepo na taarifa kumhusu anayetajwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, pamoja na wanachama wao zaidi ya 60, kuwa wamehamia Chama Cha Mapinduzi CCM na kupokelewa na Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Ni upi uhalisia wa taarifa hii inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa wanaotajwa kuwa viongozi wa CHADEMA ngazi ya mwenyekiti Ngugu Terry Kilugala na nafasi ya katibu Ndugu Gershom Migasa Mipawa katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu si viongozi wa CHADEMA katika wilaya ya Itilima kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa.
Aidha, matokeo ya Uchaguzi wa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Itilima yaliyotangazwa mnamo tarehe 20/12/2023 yanaonesha kuwa aliyeshinda nafasi ya uenyekiti alikuwa ni JACKSON SCANIA LUYOMBYA akipata kura 169 akimshinda Telly Kilugala Maduhu aliyeshika nafasi ya pili kwa kura 27.
Katika nafasi ya katibu aliyekuwa ameshinda alikuwa ni NASORO MAGNA GOSHALIMI akipata kura 124 huku John Maduhu Ndongo akifuatia kwa kura 98 na Mishali Nelcon Gegema akipata kura 9.
Vilevile, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya nje CHADEMA, John Mrema amekanusha taarifa inayodai Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Itilima na viongozi wengine kuhama CHADEMA na kujiunga CCM.
Adha ameeleza kuwa Mweneyekiti Wilaya Itilima ni JACKSON SCANIA LUYOMBYA na Si Terry Kilugala kama ambavyo Taarifa kutoka akaunti Rasmi ya CCM zinadai.
Akizungumza na JamiiCheck,
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu, Musa Onesmo amesema "Taarifa za kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Itilima amehamia CCM ni za Uongo. Aliyehamia CCM wala siyo kiongozi wa CHADEMA."