Mwenyekiti na Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yawapasa mjiuzulu nyadhifa mlizochaguliwa na wapiga kura wenu kutoka

Mwenyekiti na Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yawapasa mjiuzulu nyadhifa mlizochaguliwa na wapiga kura wenu kutoka

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Bila kukupesa macho niende moja kwa moja kwenye pointi hapo juu Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza.

UWT ni umoja wa wanawake Tanzania hakika ni moja Kati ya jumuiya yenye nguvu kubwa sana katika Chama Cha mapinduzi maana wanawake ni jeshi kubwa.

Nimesikitishwa sana siku ya wanawake duniani, maadhimisho yaliyofanyika tar 8/3/2023. Umoja wa wanawake Tanzania ya chama cha mapinduzi kuwa kimya Kama kimepatwa na msiba mzito.

Bali siku hiyo ilisikika BAWACHA ambayo ni Baraza la wanawake Tanzania huku UWT wakiwa kimya Kama vile mtu aliye mwagiwa maji ya baridi.

Katibu taifa, mwenyekiti taifa kwa hiki kilichotokea nakufanya jumuiya ya akina mama CCM kutosikika katika maadhimisho ya wanawake duniani hakika huu ni uzembe mkubwa sana yawapasa mjiuzuru Mara moja hiyo nyazifa mliyopewa na wapiga kura wakiamini kuwa mtawawakilisha vizuri nakufanya jumuiya kuwa hai nakusikika kimataifa.

Mwenyekiti, na katibu taifa kwa masirahi mapana ya jumuiya ya akina mama mnapaswa mjiuzuru wachaguliwe watu wenye kujua mantiki yakuwepo hapo.

Nimeandika haya kwa uchungu sana kijana mnyenyekevu ndani ya chama changu Cha ccm na mwanachama hai kabisa ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom