Pre GE2025 Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti CHADEMA ni paka na panya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe PendoLyimo nitafute kama kuna shida
 
Kuna gazeti lilikua linamilikiwa na jamaa mmoja wakati wa magufuli na ndio lilikua na vichwa vya habari za namna hii. Unajua mpaka Leo jamaa anadaiwa mabilion ya fedha.

Kazi ya toilet paper ni kuondoa uchafu sehemu nyeti baada ya hapo halipaswi kushikwa na yeyote. Tafakari
 
 
MALAYA WA KISIASA KAZINI ...GAZETI LENYEWE HILO KUQQQUMA YAKO .
 
jamaa gani tena huyo , si mtaje
 
Wakati migogoro hii ya ndani ikiendelea kuonekana hadharani, swali linabaki: Je, CHADEMA inaweza kunusurika na dhoruba hii, au anguko la chama hicho linakaribia?
Umesomeka na kueleweka, ingawa alama za vurugu ndani ya CHADEMA hazikuanza leo na huo unaouita "wizi wa Mbowe'.
Alama zimekuwepo toka Mbowe alipo tolewa gerezani, na siku hiyo hiyo, kwenda nyumbani kuvalia suti na kuelekea Ikulu.
Zile habari za mazungumzo ya "Maridhiano"; bila shaka kazi hiyo matokeo yake ni pamoja na haya yanayo shuhudiwa sasa hivi ndani ya CHADEMA.

Kwa hiyo, tokea wakati huo wa kutoka gerezani, Mbowe ni kama aliye ingizwa kwenye dini mpya, kapata ubatizo/kaslimu upya katika dini yake hiyo mpya.

Wewe umetazama upande mmoja tu wa sarafu, unao ihusu CHADEMA, lakini hukutaka kujihusisha vyovyote vile na nafasi ya CCM katika jambo hili; na wala huoni haja ya kuzungumzia hali ya huko ndani ya CCM yenyewe, pengine kwa kukosa nafasi ya kutosha katika andiko lako ili lisomeke kwa urahisi na kueleweka.

Kwa hiyo, mimi ninakusihi, utakapo pata nafasi nzuri, baada ya kutuliza akili vizuri, jaribu kudadisi yafuatayo:
Kwa mfano- kama CHADEMA wanavurugika, tena kwenye saa mbaya hii, nani hasa anaye weza kuwa anachochea moto huo unao waunguza CHADEMA, na sababu zake ni zipi? Inawezekana lengo likawa ni kumvuta Mbowe, awe Raila Odinga wa Kenya kwa Samia wa CCM, ambaye naye atakuwa hatarini kuvurugwa na kundi la Magufuli?

Ningependa kuendelea, lakini yatazame hayo kwanza kwa sasa kwanza.
 
Unatumia vibaya jina la Lyimo πŸ™‚ πŸ™‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…