Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa iliyopo Kata ya Bonyokwa katika Manispaa ya Ilala anatuhumiwa kushirikiana na baadhi ya Polisi ambao sio waaminifu kutoka Kituo cha Polisi cha Stakshari kuwalinda wahalifu ambao wameendelea kufanya uhalifu Kwa wananchi wa Mtaa huo .
Mwenyekiti ambaye anajulikana kwa jina la Maliyataabu amekuwa akienda Polisi na kuwawekea dhamana wahalifu ambao wamekuwa wakikamatwa na Jeshi la Polisi kwani miongoni mwa wahalifu hao wapo nduguzake ambao wanahusika na uhalifu wa kupora,kukata watu mapanga na kuwateka watoto ambao wanakuwa wanapita njiani Kwa kuwataka watoe fedha wawapo njiani.
Mathalani, Ijumaa iliyopita Polisi walifanya msako na kuwakamata vijana 11 ambao walikuwa kwenye kijiwe cha wavuta bangi ambacho kipo karibu kabisa na Kanisa la KKKT Bonyokwa nyuma ya stendi ya Bonyokwa, Jambo la kushangaza NI kuwa wahalifu hao waliachiwa siku ya jumapili jioni baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo kwenda kuwawekea dhamana Kituo cha Polisi Stakshari.
Hali ya uhalifu katika Mtaa huo imekuwa mbaya Kwa watu mbalimbali kuvamiwa nyakati za asubuhi na usiku ,nyumba kuvamiwa na kuvunjwa milango na madirisha na Mali kuporwa,wanawake na wanafunzi kuvamiwa alfajiri wanapokuwa wanaenda kazini na mashuleni na kukatwa mapanga mara Kwa mara, wafanyabiashara hulazimika kufunga huduma kabla ya saa Nne usiku kutokana na usalama mdogo!
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala na Kanda Maalum ya DSM wanapaswa kufanya uchunguzi wa kina na kama wanataka pa kuanzia wazungumze na vijana wa bodaboda ambao wamekuwa wakitoa taarifa za wahalifu na hakuna hatua zaidi ya Mwenyekiti wa Mtaa kwenda kuwajulisja wahalifu hao kuwa ni akina Nani wanaotoa taarifa juu ya uhalifu huo.
Bangi inauzwa kwenye Mabanda yaliyopo Bonyokwa stendi kama bidhaa Halali na wanaouza hawakamatwi na inapotokea mmoja amekamatwa wenzake huchangishana fedha na kutoa rushwa kuanzia Serikali ya Mtaa mpaka Polisi Stakshari na kuhakikisha kuwa wanaachiwa bila kufikishwa Mahakamani pamoja na kukamatwa na ushahidi wa kutosha .
Mtaa wa Bonyokwa wapo maafisa wa Jeshi la Wananchi ambao nyumba zao zimevamiwa na kuvunjwa milango wawapo kazini na hakuna msaada wanaopata zaidi ya kujikuta wanalalamika Kwa mamlaka za kiraia na hakuna hatua madhubuti ambazo zinachukuliwa .
ZCO wa Kanda Maalum anapaswa kuchukua hatua stahiki mapema iwezekanavyo kabla Mtaa huo haujatangazwa rasmi kuwa makazi mapya ya wahalifu katika Jiji la DSM na kusababisha Hali isiyodhibitika siku za usoni!
Nitaendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu nitawataja Kwa majina wahalifu na Polisi ambao wanashirikiana nao siku sio nyingi ! Naazima Maneno ya Mwanakijiji wa kale kuwa Inzi Yuko kazini huko Bonyokwa na Stakshari Polisi!
Stay tuned !