Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma ( UVCCM) Abdulhabib Mwanyemba, amewahimiza Vijana nchini wakiwemo wa CCM kujitokeza kwenda kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kupiga kura itakapofika kipindi cha uchaguzi.
Mwanyemba ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika Kijiji Cha Machali wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambapo ameongozana na kamati ya utekelezaji ya UVCCM ya mkoa na wilaya.