Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wilayani Nyangh'wale Mkoani Geita wameaswa kutojiusisha na Vitendo vinavyoweza kupelekea kuvunja amani sambamba na kutojihusisha na Shughuli za kiuhalifu .
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Geita , Manjale Magambo wakati alipofanya ziara ya wilayani humo na kugawa Reflecta huku akiwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za Mikopo ya asilimia kumi sambamba na vijana kushiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu 2025.