Pre GE2025 Mwenyekiti UVCCM Geita: Hatufurahishwi kuona vijana wetu wanaondoka duniani kwa kutekwa! Tunalaani na kukemea matendo haya!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Naona suala la utekaji limekuwa ni suala gumu mno imefikia hatua hadi CCM wameanza kupiga kelele.

CCM tulieni. Kila mtu atafikiwa kwa wakati wake.

Haya makelele Chadema walianza mapema kulalamika kuhusu utekaji mkawaona hamnazo, jamii imekaa kimyaa kama haiwahusu vile.

Naona sasa hii ngoma tumeanza icheza wote sasa

=================================

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, amelaani vikali vitendo vya utekaji vinavyoripotiwa katika msitu wa kutoka Geita kuelekea kata za Bugulula, Kamhanga, na Nyawilimilwa, ambavyo vimeendelea kusababisha majeraha na vifo kwa wananchi.

Akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM katika kata za Kamhanga, Bugulula, na Bugarama, Manjale alisema kuwa chama na vijana hawakubaliani na matukio yanayoleta madhara kwa wananchi, hasa yale yanayopelekea upotevu wa maisha.

Baadhi ya wananchi, akiwemo Methusela Mpina na Joseph Juma, walisema kuwa hali hiyo imewafanya waishi kwa hofu kutokana na kushuhudia visa vya utekaji mara kwa mara katika eneo hilo.

Kutokana na malalamiko hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Sophia Jonge, ameeleza mikakati ya kuhakikisha usalama wa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha doria za mara kwa mara katika eneo hilo.

Kwani wanatekwa na nani?. Mbona anajiweka kimabano
 
Wameanza kushituka Sasa hivi??
Too late!
 
Back
Top Bottom