Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, amewataka wanachama wa chama hicho kutokata tamaa au kununa pale wanaposhindwa kwenye kura za maoni.
Manjale amesema kuwa, kushindwa kwenye kura za maoni hakumaanishi mwisho wa safari, bali ni fursa ya kujitathmini na kuendelea kukijenga chama cha Mapinduzi.
Ametoa kauli hiyo akiwa katika Jimbo la Bukombe katika mwendelezo wa ziara ya kamati ya utekelezaji (UVCCM) ambapo amesisitiza kuwa, kuna baadhi ya watu wana tabia ya kutafuta njia ya kutokea pindi wanaposhindwa, lakini kwa wale walio na nia ya dhati ya kushiriki katika maendeleo ya chama, wanapaswa kubaki imara na kuendelea kujenga chama pamoja.
‘’Ukipigwa kwenye kura za maoni hakuna haja ya kununa, kuna watu wanatabia wakishapigwa kwenye kura za maoni wanatafuta mlango wa kutokea, ukipigwa baki humuhumu tukijenge chama chetu…acha mambo ya kununanuna unataka uwe wewe tu.