SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Nimefuatilia mjadala wote humu, ninachoweza kusema baada ya kutafakari kwa kina kwa kuwa na Mimi ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya... Wenyeviti huwa tunaumizwa sana na baadhi ya watendaji wetu pamoja na Viongozi wetu ndani ya kamati za utekelezaji na Idara...
Niweke kumbukumbu sawa kwa kusema wazi kuwa Wilayani kwangu wote tunaheshimiana na tunafanya kazi vizuri sana na Viongozi wenzangu... Lakini nimewahi kubadilishana uzoefu na baadhi ya wenyeviti wenzangu wakijaribu kuonyesha changamoto wanazo kutana Nazo, nimejaribu kulinganisha hiyo taarifa na baadhi ya Changamoto zinazo wakumba wenyeviti wenzangu wa Wilaya... Naona kabisa zinaweza kuwa na ulinganifu na UVCCM Makao makuu.
Mara nyingi wanao sumbua jumuiya ni King makers, wakishafanikisha kukuweka madarakani kinachofuata huwa wanataka idara zote zishikwe na watu wao, kwa hiyo Mwenyekiti unapangiwa safu nzima [emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivyo kila utakachofanya ni lazima uzingatie maslahi yao, ukienda kinyume kitakacho fuata ni fitina na vurugu... CCM inataratibu zake za kuonyana na kuwekana sawa, wameshindwa nini? Kutumia vikao kumaliza haya mambo mpaka kuamua kwenda kwenye gazeti la upinzani kuvuana nguo?
Kimsingi vurugu zote zinazotokea ndani ya Jumuiya iwe ngazi ya wilaya au Mkoa, huwa zinasababishwa na sisi viongozi ndani ya Jumuiya tukisaidiwa na Viongozi wengine walioko nje ya jumuiya kwa kuwaelekeza watu wao walioko ndani ya Jumuiya kukwamisha mambo..
Hembu sisi maamuma tujiulize, mwandishi anasema amewasiliana na baadhi ya Vigogo makao makuu wametoa ufafanuzi wao kisha wanasema itapendeza Mkiwauliza Mwenyekiti na Katibu kwani ndio watuhumiwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787] hii inaashiria hapo mjengoni hakuna uelewano anatafutwa mtu wa kutolewa kafara
Sina shaka na utendaji wa Mwenyekiti wangu wa Taifa, bundi unawafuga wewe, baraza likusaidie kufumua idara zote makao makuu upange safu upya ili uwasaidie Vijana wa Taifa hili...
Huwa najiuliza Mara nyingi kwa mini Mbunge flani kutoka Mkoa wa Tabora huwa hakosi kualikwa kwenye baraza Taifa? Kuna nini? Wapo Viongozi waliojenga heshima ya UVCCM kama akina Martin Shigela, lakini sioni akipewa heshima hiyo kama huyu Mheshimiwa anavyopewa.
Rai yangu, Viongozi wenzangu tuache majungu tujenge Jumuiya.
Ayoub Bindulle Maandazi
M/kiti UVCCM WILAYA YA MAGU
Sent using Jamii Forums mobile app